Ni miaka ya 90.Kitu tunachokiita hivi leo Bongo Fleva ndio kwanza kinaanza kushika kasi. Hakikubaliki bado. Wazazi wengi wanasema ni uhuni.Rap,Rap.Maanake nini? Vijana hawaeleweki mbele ya wazazi,ndugu,jamaa na hata baadhi ya marafiki. Yule keshapotea. Siku hizi kila ukikutana naye anarap-rap tu. Pamoja na hayo, zipo sehemu wanazokubalika. Kuna party za ufukweni. Huko wapo watu wanaowaelewa na kuwasikiliza achilia mbali kuwaona “idols”. Hawakukata tamaa. Wakaendelea kujitoa muhanga kwa kuelimisha kupitia sanaa ya muziki. Leo hii, muziki upo ulipo. Unasikilizwa na watu wa rika zote. Kampeni zinaendeshwa zikisindikizwa na muziki huo.
Miongoni mwa vijana waliokuwepo katika kundi hilo la ‘waasisi” ni pamoja na Ahmed Dola (pichani) ambaye kwa jina la kisanii, anajulikana kama Balozi Dola Soul. Bila shaka unamkumbuka toka enzi zile za The Deplomatz. Alitamba sana na nyimbo kama vile Kwenye Chati, Nje ya Ndoa (akishirikiana na Mabaga Fresh) na zinginezo kibao.
Baada ya mafanikio kadhaa katika muziki ikiwemo tuzo ya kundi bora la Hip Hop akiwa na The Deplomatz mwaka 1999, Balozi aliamua kuhamishia makazi yake nje ya nchi akipitia nchi kama Uingereza na hatimaye Marekani alipo hivi sasa.
Je,amekacha game moja kwa moja? Jibu la wazi ni Hapana. He was busy taking care of other things such as school and family. Now he is back. Anawakumbusha wapenzi wa Bongo Fleva, toka katika generation yake mpaka hii mpya, kwamba bado anaweza na yupo tayari kurejea. Wimbo unaitwa Balozi Wenu.!!
No comments:
Post a Comment