b..

B1

Wynem

animation

Monday, September 28, 2015

TIMU 'NIMESTUKA' ILIVYOFANYA MAMBO DODOMA MJINI

Juma nature na Inspekta Haarun na wasanii wengine wakiwa wanaingia katika viwanja vya Mnadani mjini dodoma.

Baadhi ya wasanii waliokuwa ukawa na kurudi Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mji wa Dodoma wakiwastua wanadodoma kustuka kuwa ukawa hakuna sera hivyo ndiomaana wameamua kurudi ccm.
Wasanii hao wanaunda timu waliyoipa jina la NIMESTUKA wanafanya kampeni za kuwastua watu katika baadhi ya mikoa ya tanzania.

Msanii Stan Bakora akisalimiana na mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini, Antony Mavunde mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Ray Kigosi akiwa na msanii mwenzake wakisalimia wananchi wa dodoma mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Juma nature na Inspekta Haarun na Rich One wakikamua katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Msanii Kitale, Ndede na Mboto wakisalimia wananchi wa dodoma mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Aunt Ezekiel akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Dodoma mjini katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Stan Bakora na Mr. Kupa wakifanya yao katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma. Picha zote na Suleiman Lyeme

Thursday, September 24, 2015

Airtel yazindua kifurushi cha “Yatosha Nyts” bila kikomo

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (kulia) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki wakionyesha bango kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kama ishara ya kuzindua huduma mpya ya kifurushi cha ‘Yatosha Nyts’ itakayomwezesha mteja kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo pamoja na kupata kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu.


Na Mwandishi Wetu
Wateja kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi bila kikomo· Piga simu bure kila siku kuanzia saa 5 usiku mpaka 12 asubuhi.

 Kwa shilingi 300 tu. Dar es Salaam,Jumatano 23 Septemba 2015, Kampuni ya simu za mikononi Airtel imewapa sababu nyingine wateja wake kufurahia usiku kwa kuwapatia “Yatosha Nyts” ofa inayowawezesha kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo,pamoja na kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu.

Ofa hii ya “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwenda mitandao yote kila siku kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi hadi siku za wikiendi.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema, “ Tunatambua wateja wetu wanamahitaji tofauti ya huduma za simu. “Yatosha Nyts” ni ofa kabambe na ya kipekee inayo kidhi mahitaji ya wateja wetu. Tumezindua “Yatosha Nyts” ofa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu ya kuwasiliana na kupanga shughuli za siku inayofuata bila hofu ya kupungukiwa na salio kwenye simu zao.

 “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja kuwasiliana na familia, marafiki , mpenzi na wafanya biashara wenzake wakati wa usiku kwa bei nafuu zaidi.

Aliongeza kwa kusema, “ikiwa ni mwendelezo wa kutoa huduma za mawasiliano bora zenye gharama nafuu, wateja wetu wanauwezo wa kununua kifurushi cha “Yatosha Nyts” wakati wowote na kuanza kufurahia kupiga simu, kutuma SMS bila kikomo na 10MB za kuperuzi.

Kwa shilingi 300 tu wateja wetu nchi nzima wanaweza kupiga simu bila kikomo Airtel kwenda Airtel , kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo kwenda mitandao yote na 10 MB za kuperuzi katika mitandao ya jamii kila usiku. Kujiunga na “Yatosha Nyts” piga *149*99#, “Yatosha Nyt” ni offa mpya na moja kati ya ofa nyingi zenye ubora ambazo Airtel inawatapia wateja wake chini ya huduma ya kibunifu ya Airtel Yatosha.

Airtel Yatosha inawapatia wateja wetu uhuru wa kununua kifurushi kinachowafaa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kutembelea sehemu za kutoa huduma.

Yatosha pia inawawezesha wateja kutengeneza kifurushi wanachokipenda, huduma ya kibunifu na ya kwanza kutoka Airtel

Friday, September 18, 2015

"NEW AUDIO" UJANA - SKYWALKER FT WAKAZI, DAMIAN SOUL, OBI ELINAMI, P THE MC, ZAIID & KICHE LEGEND


Pata picha wanapokutanishwa rappers wakali watano na waimbaji wawili mashuhuri wa R&B kwenye wimbo mmoja! Matokeo yake utayafahamu zaidi pale utakapotenga dakika zaidi nne kuusikiliza wimbo huu ambao hauishi kuwa na ujumbe muhimu tu, bali wenye mdundo wa kuvutia, mashairi makali na style za kutofautiana za uchanaji pamoja na melody tamu za R&B.
Wimbo huu uliotayarishwa na Skywalker unazungumzia ndoto chanya za vijana wanaotumia nguvu, elimu na vipaji vya kujitengenezea maisha yao mazuri sasa na sio baadaye. Ujana ni wimbo unaowakumbusha vijana kuwa wakati wa kutafuta maisha mazuri ndio huu na kila mmoja anapaswa kuchangamka.

VERSE 1 BY P THE MC

P ni zao za Tamaduni Muzik na kwa wale mashabiki wanaohudhuria vilinge vya Msasani Club watakuwa wanajua uwezo wake. Hadi sasa ameshaachia zaidi ya nyimbo 30 ambazo zinapatikana kwenye akaunti yake ya Mkito. Kwa ushirikiana na Zaiid, waliachia mixtape yao iitwayo Mwenge Kiwalani. Hivi karibuni aliachia ngoma yake ‘Run DSM’ aliyowashirikisha Dully Sykes na Young Killer.

VERSE 2 BY OBI ELINAMI

Obi ni muimbaji wa R&B na producer ambaye kutokana na kazi zake za corporate zimemfanya asijulikane sana lakini uwezo wake si wa kuelezeka kirahisi. Pamoja na kuachia ngoma zake mwenyewe zikiwemo Lost, Right/Left, Far Away na Nilipokuona amekuwa akifanya cover za wasanii wa nje ukiwemo ‘I'm Not The Only One’ wa Sam Smith.

VERSE 3 BY WAKAZI

Wakazi ni miongoni mwa rappers wa Tanzania wenye mixtapes nyingi zaidi za hip hop zikiwemo tatu za MYU: The Trilogy, Abacus EP na Live From Stakishari. Anatarajia kuachia album yake mpya iitwayo Kisimani.

VERSE 4 BY ZAIID

Hili ni zao lingine la Tamaduni Muzik. Zaiid alijipatia sifa zaidi pale alipoachia cover ya wimbo wa J.Cole, Who Dat. Mwaka 2013 aliachia mixtape yake iitwayo KANDA MBOVU. Yeye na P The MC wana mixtape yao ya pamoja, Mwenge Kiwalani. Hivi karibuni aliachia cover ya wimbo wa Fetty Wap ‘Trap Queen’ aliyoipa jina ‘Madebe.’

VERSE 5 BY DAMIAN SOUL

Damian alianza kufahamika kutoka kwenye mashindano ya Tusker Project Fame kabla ya kuanzisha career yake kama solo artist. Amefanikiwa kutoa hits kadhaa zikiwemo Ni Penzi na Baraka alizomshirikisha Joh Makini na wimbo wake wa sasa ‘Tudumishe’ aliomshirikisha G-Nako. Mwaka jana alikuwa mmoja wa wasanii walioshiriki kwenye shindano la Maisha Superstar.

VERSE 6 BY SKYWALKER

Sky ni mtangazaji wa redio, mhariri wa tovuti ya burudani ya Bongo5.com na producer pia. Amewahi kutoa mixtape yake iitwayo Nimefunzwa.

VERSE 7 BY KICHE LEGEND

Kiche ni kiongozi wa kundi la vijana watano liitwalo 909 wenye nyimbo kama Angalia Juu, Sikubaliwa Kushindwa na Njoo Hapa.

UNAWEZA PIA KUDOWNLOAD WIMBO HUU KWENYE LINK HII: http://bit.ly/1KiDHKH 

Tuesday, September 8, 2015

FLAVIANA MATATA APEWA UBALOZI WA UTAALI

Mwanamitindo wa Kimataifa anaefanyia kazi zake za nchini Marekani Flaviana Matata amechagulia na Wizara ya Maliasili kuwa Balozi wa Hiyari 'Good Will Ambassador' kwa kipindi cha miaka mitatu kwa dhumuni la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.

 Dr Adelhelm James Meru akimkabidhi Flaviana Matata barua ya kuchaguliwa kwake huku kaimu Mkurugenzi Devota Mdachi akishuhudia, katika ofisi za wizara hiyo

Flaviana ambaye juzi alikuwa mmoja kati ya shuhuda wa kushuhudia wizara ya maliasili na utalii wakizindua rasmi tangazo litakalokuwa linatangaza vivutio vya Tanzania nje ya anchi alitawazwa leo hii na katibu mkuu Dr Adelhelm James Meru aliyemkabidhi kwa niaba ya Waziri , Mheshimiwa Lazaro Nyalandu huku Kaimu Mkurugenzi Madam Devota Mdachi akishuhudia.

Tuesday, August 11, 2015

WASANII WATAKIWA KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kushoto) akifuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa na watoto wanaondaliwa na Baraza hilo kupitia programu ya ‘Sanaa kwa Watoto’ wakati wakitumbuiza kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Watoto hao wanatoka shule ya Msingi ya Msimbazi iliyoko Ilala jijini Dar es Salaam. Katikati ni Msanii wa filamu Honeymoon Mohamed na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Stadi za wasanii Bi. Vick Temu.  

Sehemu ya watoto wanaoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia programu yake ya Sanaa kwa Watoto wakicheza igizo kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Watoto hao wanaosoma Shule ya Msingi Msimbazi walikuwa kivutio kikubwa kwa wadau wa Sanaa. 

Wasanii kutoka Kundi la Ngoma za Asili na Maigizo la Jivunie lenye  makazi yake eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wakionesha ufundi wao katika kuchenza ngoma za asili kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba kwa mwezi mara mbili siku za Jumatatu.



Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wametakiwa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida wanayoipata kupitia kazi zao za Sanaa kwa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji maalum ili kujijengea mtandao wa kudumu wa masoko, uhalali na taswira nzuri kwa jamii.
Wito huo umetolewa mapema wiki hii na mtengeneza filamu wa Tanzania mwenye makazi yake nchini Marekani Bi. Honeymoon Mohamed wakati akiwasilisha mada kuhusu Filamu za Kitanzania na Masoko kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa inayoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
“Wasanii wanaitegemea jamii kama chanzo cha mapato yao hivyo ni lazima wajenge utamaduni wa kurejesha kile kidogo wanachokivuna kutoka kwa jamii kupitia kusaidia watu wenye uhitaji maalum” alisema Honeymoon ambaye filamu yake ya Daddy’s Wedding  imeshinda tuzo kwenye tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar (ZIFF) lililomalizika hivi karibuni eneo la Ngome Kongwe, Zanzibar. 
Aliongeza kwamba watoto wenye uhitaji maalum wanapata faraja na kuhisi kupendwa na jamii pale wanapotembelewa mara kwa mara na watu mbalimbali wenye umaarufu na nafasi kubwa katika jamii hivyo wasanii wetu hawana budi kuwa sehemu ya kujenga faraja hii kwa watoto hawa.
Kwa mujibu wa Honeymoon wasanii wa Tanzania wako nyuma katika kuikumbuka jamii hususani kutembelea makazi ya watoto wenye uhitaji maalumu na kuchangia huduma mbalimbali zinazokuwa zinahitajika.
“Watoto wenye utindio wa ubongo wako wengi, kuna wale wenye ulemavu wa ngozi na wengine wanaishi wakiwa yatima kwenye vituo mbalimbali lakini wasanii wetu wamekuwa wazito kuwakumbuka. Wasanii hawana budi kuyakumbuka makundi haya maana wako kwa ajili ya jamii” alisisitiza.
Awali kabla ya uwasilishaji wa mada hiyo, watoto wanaoandaliwa kupitia programu ya BASATA ya ‘Sanaa kwa Watoto’ kutoka Shule ya Msingi wa Msimbazi iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam walitoa burudani mbalimbali za Sanaa wakisaidiana na Kikundi cha Sanaa cha Jivunie chenye maskani yake neo la Mbagala Manispaa ya Temeke.

Sunday, August 9, 2015

MISS KILIMANJARO AMBASSADOR 2015 YOLANDA SHAYO AINGIZWA MITINI NA MUANDAJI

Mshindi wa Miss Kilimanjaro 2015, Yolanda shayo


Na Mwandishi Wetu
Muandaji wa shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015, Jackline Chuwa adaiwa kuingia mitini na fedha za zawadi za warembo na malipo kwa watu aliofanya nao kazi kufanikisha shindano hilo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya familia ya mshindi wa shindano hilo zinasema kuwa vikao vya mara kwa mara hufanyika kupanga mkakati wa kuvamia ofisi za BASATA kujua hatma ya binti yao Yolanda shayo.

ILIKUAJE:
Wakati wa kutangaza matokeo ya ushindi siku ya fainali za mashindano hayo usiku wa julai 24,mshindi alikabidhiwa Televisheni kama zawadi na kiasi cha pesa kilichoadiwa kutolewa na mdhamini mkuu ambae ni Coca cola.
Cha kustaajabisha muandaji huyo alienda ofisi za kampuni hiyo na kuchukua kiasi hiko cha fedha ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza lakini mpaka leo mrembo huyo anahaha kupata zawadi yake.
Yolanda aliamua kufunga safari mpaka ofisi za Bonite Bottles na kuwauliza wahusika kuhusu zawadi yake na alijibiwa kuwa muandaji huyo alishakabidhiwa fedha hizo siku nyingi.
Mrembo huyo alichukua hatua nyingine ya kumpigia simu Jackline na kumuulizia kuhusu zawadi yake ya fedha taslimu alioadiwa jukwaani na wadhamini wakuu,chakushangaza muandaaji huyo alitoa kauli ya kumvunja moyo kwa maana hatoipata kabisa kwa kisingizio eti hakupata faida.

FAMILIA YA YOLANDA:
Familia ya mrembo huyo imechukizwa na kitendo cha muandaaji huyo kwa kuingia mitini na zawadi ya binti yao na bila kumkabidhi mikononi mwa kampuni hiyo ambapo ilitoka ahadi kuwa atakuwa balozi wa kampuni hiyo kufanya kazi mbalimbali kama balozi wa kinywaji hiko mkoani humo.
Wazazi wa mrembo huyo wamedhamilia kutinga ofisi za BASATA kufatilia mkataba wa bitni yao kutokana hali ya sintofahamu kuendela toka binti yao atawazwe kuwa mshindi mnamo julai 24.
Pia wanafamilia wametoa shutuma nzito kwa shindano hilo wakihoji ni kwanini  msanii wa bongo flava anapewa milioni 25 kutumbuiza wakati binti yao ambae ndiye mshindi anambulia zawadi ya televisheni pekee.

WASHIRIKI WENGINE:
Hali ni tata pia kwa washiriki wa walioingia tano bora hasa namba nne ambae alizawadiwa laki nne na mapazia kutoka kampuni ya Mapazia house lakini chakushangaza muandaji huyo aliingia mitini na fedha hizo na kumuacha mrembo akirudi nyumbani na mapazia tu.
Mrembo huyo Willice Donard amelalamikia kitendo cha muandaji huyo kumjibu majibu ya dharau pale alipompigia simu kuulizia zawadi yake.
Habari zinasema kuwa mrembo alieshika namba tano,Femy Lema alipokonywa nusu ya kiasi cha fedha alichokabidhiwa jukwaani ikiwa ni zawadi ya kuingia tano bora.

KAMATI YA MAANDALIZI:
Hali si shwali kwa upande wa kamati,habari za uhakika toka  kwa watu walioshiriki kumpa sapoti muandaaji huyo zikizadai kuwa amewaingiza chaka na kuwazulumu haki yao ya malipo,mpaka sasa hawajui fedha zao watazipataje.
 
KAULI ZA MUANDAAJI:
Kauli za muandaji zilizojaa dharau na kejeli kwa watu wanaodai haki zao ndizo zilizowapandisha hasira na kufanya baadhi ya watu kutoboa ukweli huu kwani amekuwa akiwaambia anaenidai aende mahakamani huko ndiko haki ya mtu hupatikana kwa kisingizio eti amesomea sheria.
 
KUMBUKUMBU ZAKE:
Kumbukumbu za muandaaji huyu zinaonesha ni mtu ambae anapenda mambo ya ujanja-ujanja na kujipatia faida kubwa kupitia majina ya watu kama alivyotaka kumtumia Zari Hassan kuvuta watu wengi kuingia katika tamasha lake na angali hakuwa na mkataba wowote na Zari.
Kitendo hiko kilimfanya Diamond Platnumz kutaka kususia na kuandika maneno makali katika ukurasa wake wa instagram,kitu kilichompelekea kutozwa faini na uongozi wa Zari.

BASATA:
Wito umetolewa kwa baraza la sanaa kuwa makini kwa kutoa vibali kwa waandaji wasio na uhakika na shughuli wanazofanya kama ilivyotokea kwenye hili shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015.
Tunaamini dhamira ya shindano hili ni nzuri na lina manufaa kwa jamii kuhusiana na utalii,utamaduni na kazi za kijamii,shindano hili lina faida ila tatizo liko kwa muandaaji mwenyewe kana kwamba hana malengo na shindano hilo.
Lawama za pekee ziende kwa Basata kwani shindano hili lilipelekwa kienyeji bila usimamizi wowote kama ilivyo kwa mashindano mengine makubwa,isitoshe kanuni na taratibu hazikufuatwa mwanzo mwisho ndiyo maana leo tunapata malalamiko ya mshindi Yolanda shayo kuingizwa mitini zawadi na mkataba wake.


TANZIA: MBUNGE WA VITI MAALUMU (CUF) - MASASI AFARIKI KWA AJALI YA GARI

Monday, August 3, 2015

YOLANDA SHAYO BALOZI WA MKOA WA KILIMANJARO ATEMBELEA VITUO VYA WATOTOTO YATIMA

 Yolanda Shayo akisaidia kugawa chakula kwa watoto na viongozi wa vituo hivyo,ambapo alishiriki kwa pamoja nao katika chakula cha mchana.

Mrembo aliebuka kidedea kwenye shindano la kumsaka barozi wa mkoa wa Kilimanjaro 2015,Yolanda Shayo ametembelea vituo vya watoto yatima katika eneo la mamba Malangu moshi vijijini.
 
Shughuli hiyo ilifanyika mapema jana ambapo mrembo huyo alitembelea vituo vinee ambavyo ni Msoroe,Mrieni,Kikoro na kotela kwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto na kula nao chakula cha pamoja kilichoandaa kwaajili ya watoto hao.
 
Baadhi ya vitu vilivyotolewa na mrembo huyo ni kalamu,madaftari,rula na sabuni za kufulia na kuogea,Yolanda alipata fulsa ya kuongea na viongozi wa vituo hivyo ambapo alibaini changamoto balimbali zinazokabili vituo hivyo.

Yolanda ambae ni Miss Kilimanjaro Ambassador wa mara ya kwanza ameonesha jitihada zake za kuanza kazi ya urembo kwa kuitumikia  jamii yake ambapo alikuwa ana wito huo tangu akiwa mtoto.
Kwa nafasi aliyoipata mrembo huyo ameaidi kuwa kinara kuutangaza utamaduni wa mkoa wa kilimanjaro na kuvitangaza kitaifa na kimataifa vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya mkoa huo.

"mbali ya kuwa mrembo na balozi wa mkoa wa kilimnjaro nitahakikisha natumia fulsa hii kupeleka ujumbe mbalimbali kwa jamii yangu ikiwemo kuwahimiza vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika octoba" aliongea Yolanda.