b..

B1

Wynem

animation

Saturday, May 14, 2011

ILIVYOKUWA JANA PALE ZONGHUA GARDEN WITH M-BAND

 
 
KAMA KAWA KUJIACHIA NA KAMERA YA MTOTO WA KITAA KAMA HIVIIIIII

Wednesday, May 11, 2011

LEO NI SIKU YA KUZALIWA MWANADADA TECLA.

Tecla ni mdau wa burudani na msanii wa muziki wa kizazi kipya. kwa sasa Tecla ni muimbaji wa bendi ya M-Band ambayo ipo chini ya mtu mzima DUKETACHEZ pale katika studio za M-Lab mitaa ya kin ondoni biafra.
SULE'S INC. & ENTERTAINMENT na timu nzima ya blog ya mtoto wa kitaa kwa pamoja wanamtakia sikukuu njema ya kuzaliwa a.k.a HAPPY B'DAY

WANNE STAR KUNOGESHA MISS ARUSHA CITY CENTER 2011.

MSANII mahiri wa ngoma za asili Tanzania, Salum Mgaya maarufu kama Wanne ‘Wanne Star’, anatarajiwa kutumbuiza katika mashindano ya kumtafuta mlimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2011 yanayotarajiwa kufanyika Mei 13 katika ukumbi wa Triple A, Arusha. Mratibu wa shindano hilo, Bi. Sophia Urio, alisema kuwa msanii huyo ataungana na kikundi cha ngoma za asili cha Kontejazz cha jijini Arusha katika kutoa burudani ambayo haitawachosha wageni waalikwa.
Mpaka sasa wamehakamilisha wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo wenye mvuto na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha. "Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri kwa sasa ni siku yenyewe ambayo walimbwende watakayochunana", alisema Bi. Sophia Urio.
Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi.
Aliongeza kuwa katika shindano hilo natarajiwa kuanza majira ya saa 2 usiku kiingilio chake kitakuwa ni shilingi 7,000/- kwa viti vya kawaida na shilindi 10,000/- kwa viti maalumu.
Alisema, wadhamini wamezidi kuongezeka na kuwataja kuwa ni pamoja na Vodacom, Startimes, Mbogo Experdistio, Litterose, Kilimanjaro Express Bus, Intelligence Security Ltd, Stone, Shuphaa Quality boutique, Janeths Beaty Parlour, klabu Santiago pamoja na Africasana Pub iliyopo Holili, Moshi.
kwa habari zaid chek na blog ya HABARI NA MATUKIO

Tuesday, May 10, 2011

BABY J: MKALI WA ZENJI ATESAYE NA TUZO LUKUKI AFUATA NYAYO ZA LADY JAY DEE.


Zanzibar wenyewe wanaita Zenj, ina wasaniii wengi wa muziki wa kizazi kipya wanaokubalika kwa kiwango kikubwa, na wanafanya vyema katika fani hiyo. Miongoni mwa wasanii hao mahiri yumo msanii wa kike aitwaye Jamila Abdallah a.k.a Baby J ambaye amekuwa akifanya vizuri na hata kujinyakulia tuzo lukuki kisiwani humo.

Msanii huyo mwenye urefu wa kiasi, kwa mara ya kwanza alianza kutambulika kwenye anga ya muziki wa bongofleva kwa wimbo wake uliotwa Mapenzi ya Kweli, aliyourekodia ndani ya studio za G Record kwa Omar Saidi Kombo a.k.a KJT, na kweli wimbo huo ulikubalika kwa wapenzi na washabiki wa muziki huo ndani ya Zenj na hata huku bara kwa kiasi kikubwa.

ASHANTI BOXI KUONESHANA UMWAMBA WA KUTUPA MASUMBWI NA MATIBWA BOXING TABATA SEGEREA.

LIGI ya kuhamasisha mchezo wa ngumi kwa mkoa wa Ilala inatarajia kufanyika tena Mei 14 kati ya mabondia wa Ashanti boxing na Matibwa ambapo ianatarajia kutimua vumbi, Tabata Segerea Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha mkuu wa timu ya Ashanti, Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye pia ni mratibu wa ligi hizo mkoa wa Ilala alisema ligi hiyo itakuwa ikifanyika maeneo tofauti ya mkoa huo ili kuweza kuhakikisha inawafikia wakazi wote wa Ilala.
Alisema, lengo hasa likiwa ni kutaka kuwavuta vijana wengi kujiunga na mchezo huo na kuepuka kukaa vijiweni huku wakiwa na kipaji cha kucheza mchezo huo ambapo mapambano ya ligi hiyo yatakuwa katika raundi nne katika uzito tofauti.
Alisema, katika mchezo huo wa hivi karibuni kwa upande wa klabu ya Ashanti mabondia watakaoenda kuchuana na mabondia hao wa Tabata ni Ibrahim clas atakae chuana katika uzito wa kg 60, Uwesu Manyota 58, Ramadhani kimangala kg 56, Rashid Mhamila kg 54, Mack Edison kg 52 na Musa Mohamed kg 49.
Alisema, kwa upande wa Ashanti wamejiandaa vizuri kiushindani kwani mabondia hao wote wapo katika kiwango cha juu hivyo wanaimani kuwaangusha mabondia wa klabu hiyo ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo.
Alisema Super D mbali ya kuamasisha mchezo wa ngumi pia kutakua na DVD zilizoandaliwa na kocha uyo kwa ajili ya kujifunza sheria za mchezo pamoja na jinsi ya kufanya mazoezi ambazo kuna mabingwa wa Dunia akiwemo manny Paquao, Floyd Maywether, Oscar Dela Hoya, Mohamedi Ally na wengine wengi.

CHEK OUT SPECIAL SONG OF MALARIA LIVE PERFORMANCE BY ALEX KAJUMULO

NOORAH AACHIA KITU CHA LUGHA GONGANA

LUGHA GONGANA umepikwa pale katika studio za B-Hits ikiwa ni mkono wake mtu mzima Hamy B. sikiliza hii ngoma hapo chini kisha Download ka vipi kwa promo tu.

Saturday, May 7, 2011

Mlab New release: Sauti ya Jogoo - Niki Mbishi Ft Maulo & bella kombo

If you carefully analyze his released songs, you will realize that NIKKI MBISHI always come with a surprise gem which later become a star. He started with his debut song “PUNCHLINES” where surprise package was GRACE MATATA (first song her voice to be heard on the radio), then his second release “KILA SIKU” which also featured by Belle 9 and Godzilla was an opportunity for the introduction of ONE THE INCREDIBLE. The third radio release material for the self proclaimed king of freestyle “PLAYABOY” was the platform for BEN POL to introduce his voice on the media. Now he is coming with the new gem “bella”. The talented singer, one of the THT rpoduct, was one of the previous BSS finalists; she is now a member of machozi band and also working on her solo album. This song was recorded early last year, by that time Bella was not on the map, Nikki is still proving that not only he is one of the best hip-hop stars of his generation but also he has a good ear. Music lab is glad to introduce his new joint “Sauti Jogoo” featuring Bella & Maulo, below are the details:

MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA 2010/2011 NI MWANAIDI HASSAN

Mtoto wa kitaa (Sule Junior) Nikifuatilia mchongo mzima wa utoaji wa tunzo za TASWA


Mgeni rasmi,Makamu wa Rais akisoma hotuba fupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tuzo za kumsaka Mwanamichezo Bora 2011,ambazo zimedhaminiwa na kampuni ya bia ya Seren
geti (SBL).

Mgeni rasmi,Makmau wa Rais
,Dr Gharib Bilal pamoja na Waziri wa Vijana,habari,utamaduni na michezo Mh.Emmanuel Nchimbi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi waliojinyakulia zawadi mbalimbali usiku wa huu kwenye hafla ya tuzo za TASWA zilizothaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti.

Mgeni rasmi,Makamu wa Rais Dr Gharib Bilal akimkabidhi tuzo kwa mchezaji wa jumla Bi.Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa netiboli katika timu ya JKT Mbweni.Mwanaidi ndiye alijijinyakulia gari aina ya Toy
ota GX 100,iliyotolewa na kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndiyo waliokuwa wadhamini wakuu wa tuzo hizo za kumsaka mwanamichezo bora wa Mwaka zilizoratibiwa na TASWA,kusho ni Waziri wa Vijana,habari,utamaduni na michezo Mh.Emmanuel Nchimbi akishuhudia tukio hilo.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa,akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali mara baada ya kuipokea tuzo yake ya heshima kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal,Mh Mkapa amesisitiza kuwa uwanja huo unapaswa uendelee kutunzwa vyema ili nchi yetu iendelee kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi vijavyo.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa, akipokea tuzo yake ya heshima kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA) kimempa mzee Kkapa tuzo hiyo maalum ya heshima, kutokana na mchango wake katika michezo hasa ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa,Mh Mkapa amesisitiza uwanja huo uendelee kutunzwa vyema ili nchi yetu iendelee kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi vijavyo,pichani kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda. Katika utoajiwa tuzo hizo mchezaji wa jumla ni Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa Netball katika timu ya JKT Mbweni.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa akipeana mkono wa pongezi na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti Breweries Ltd,Teddy Mapunda kwa kudhamini tuzo hizo za kuwapa heshima na kuwathamini wanamichezo wetu hapa nchini.Anaeshuhudia kwa nyuma ni Mgeni Rasmi,Makamu wa rais Dr Gharib Bilal.

Mwenyekiti wa bodi ya Serengeti (SBL),Mzee Marck Boman akimkabidhi tuzo mchezaji bora wa kiume wa timu ya Yanga Shadrack Nsajigwa.

Meza Kuu ikiwa imechangamka,hapa ilikuwa ikifurahia jambo kutoka jukwaani.

Mwenyekiti wa chama cha Michezo (TASWA),Juma Pinto akizunguma mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia uto
aji tuzo kwa wanamichezo mbalimbali akiwemo na mwanamichezo bora kwa ujumla usiku huu ndani ya hotel ya Movernpick,jijini Dar.


Thursday, May 5, 2011

P WISE AACHIA VIDEO YAKE YA KWANZA

Ngoma hii (NAHITAJI) kutoka kwa msanii P WISE ft Q Jay imetengenezwa pale M Lab ikiwa ni mkono mzito kutoka kwa WILLIE HD na video ikiwa imepikwa pale Mega Pix 20 chini ya SUMA MNAZALET

HII NI KWA WATOTO WA KITANZANIA WANAO TAKA KUCHEZA MPIRA KWENYE CLUB YA MPIRA YA KAJUMULO FC

KAMA KUNA WATOTO WA KITANZANIA WANAO TAKA KUCHEZA MPIRA KWENYE CLUB YA MPIRA YA KAJUMULO FC  WANAWEZA KUJIUNGA WATOTO WAWE WENYE MIAKA 10 - 16 KILA TIMU TUNATOA NAFASI MBILI KWA WAZAZI WA SIO NA KIPATO CHA KUTOSHA. NA NITAJITOLEA KAMA NI WATOTO WA KITANZANIA NITATOA NAFASI BULE KILA TIMU WATOTO WA 4 BULE .THENKX ONE LOVE IS LAW.



KAJUMULO FC
GU13 Farasi ‘98
Head Coach, Alex Kajumulo
• Coaching Experience: 1996-present
• October 2000- Ghana “A” Coaching License
• Feb. 2000 Technical and Tactical training Certificate
Brazilian Football Academy, Rio de Janeiro, Brazil
• November 1999 Course of Modern Brazilian Football for Foreign Trainers and Coaches
• FIFA Official Technical Instructor, Brazilian Football Academy, Rio de Janeiro, Brazil
Kajumulo FC is a select soccer club affiliated with Seattle Soccer Club and US Club. Our teams
play in the Puget Sound Premier League and practice in north Seattle. We offer unique skills
development programs in a positive team environment that emphasize fun because players who
have fun love to play. Our coaches have international playing and coaching experience. They live
for soccer! We are looking for highly motivated and dedicated soccer players who love soccer
and are willing to work hard to build success for themselves and their team. Join us for practice
and see if our program is right for you!
During May we will be having open practices on Mondays and Wednesdays from 4:00 to 5:30 at
View Ridge Playfield
Anticipated Costs
$ 1450 Training, league dues, fields, tournaments
$ 55 Uniforms
Two scholarships available per team
For more information and registration information, please contact:
Steve Murray (206)369-0305 steve.murray@rmiondemand.com
Please check out our affiliated Soccer Monster Training Academy


Tuesday, May 3, 2011

DOWNLOAD NGOMA YA Young Dee Ft Mataluma, Kitokololo, Chekedaa - Tunapeta (For Promo Only

Brand new song by Young Rapper Young Dee.

KAMBI YA ILALA YAMPA SAPOTI BONDIA MBWANA NA KUMSAMBALATISHA MKENYA


Bondia Mbwana Matumla (kulia) akipambana na Gabriel Ochueng wa Kenya wakati wa pambano lake la kugombania ubingwa wa UBO Mbwana alishinda kwa pointi wakati wa pambano ilo la ubingwa wake lililipigwa raundi 12 na kufanikiwa kumnyuka mkenya huyo.
Damu nzito kuliko maja bondia mkongwe Rashidi Matumla (kulia) akimpatia maelezo mdogo wake Mbwana Matumla wakati wa pambano lake la kutetea Ubingwa wa UBO lililofanyika Dar es salaam jana Mbwana alishinda kwa point na kutetea vema rtaji lake kushoto ni kocha Habibu Kinyogori.
Mbwana Matumla akikabidhi mkanda wake mara baada ya kumchapa Gabriel Ochueng wa Kenya wakati wa pambano lake la kugombania ubingwa wa UBO Mbwana alishinda kwa pointi wakati wa pambano ilo la ubingwa wake lililipigwa raundi 12 na kufanikiwa kumnyuka mkenya huyo.

Monday, May 2, 2011

VODACOM MISS ARUSHA CITY CENTER KUZINDULIWA LEO

Hii ndio nembo mpya ya Vodacom Miss Tanzania

Mashindano ya ulimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Vodacom Miss ArushaCity Center 2011 yanatarajiwa kuzinduliwa kesho Mei 2 katika ukumbi wa Via Via jijini Arusha.

Akizungumza na blog hili, mraribu wa shindano hilo Bi. Sophia Urio alisema kuwa kwa sasa wamejiandaa vyema tayari kwa ajili ya kufanya uzinduzi huo na mashindano hayo rasmi yatafanyika Mei 13 katika Ukumbi wa Triple A jijini humo.Mpaka sasa wamehakamilisha wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo wenye mvuto na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha.



"Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri kwa sasa ni uzinduzi wa mashindano hayo ili tuweze kuendelea na kila kitu," alisema Bi. Sophia Urio.
Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi. 
Wadhamini katika shindano hilo ni Vodacom, Startimes, Stone, Shuphaa Quality boutique, Janeths Beaty Parlour pamoja na Africasana Pub iliyopo Holili, Moshi.

Sunday, May 1, 2011

VODACOM MISS TANZANIA ILIVYOZINDULIWA JIJINI DAR.

Hivi ndivyo nembo ya Vodacom Miss Tanzania 2011 itakavyokuwa,ilizinduliwa rasmi hapo jana katika Hotel ya kimataifa ya Kilimanjaro Kempnsiky jijini Dares Salaam

Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya itakayotumika katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 na shindano hilo kuzinduliwa rasmi hapo jana katika Hotel ya kimataifa ya Kilimanjaro Kempnsiky wengine ni baadhi ya warembo waliowahi kushiriki katika kinyang’anyiro cha Vodacom miss Tanzania miaka iliyopita.

Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akiwasalimu baadhi ya warembo waliowahi kushiriki katika kinyang’anyiro cha Vodacom miss Tanzania miaka iliyopita ,katika uzinduzi rasmi wa Vodacom Miss Tanzania 2011 uliofanyioka hapop jana katika Hotel ya Kilimanjaro Kempnsiiky.
Baadhi ya vimwana vilivyowahi kushiriki katika shindano la Vodacom miss Tanzania 2010 ambapo Genevieve Emmanuel kushoto ndiye alinyakuwa taji la Vodacom Miss Tanzania 2010 nao walikwepo katika uzinduzi huo.
Baadhi ya kamati ya Vodacom Miss Tanzania pamoja na wadhamini wakuu wa shindano hilo na warembo waliowahi kushiriki katika shindano la Vodacom miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Lino Internation Agency waandaji wa Miss Tanzania Hashimu Lundenga akiongea na kuwatambulisha baadhi ya warembo waliowahi kushiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania miaka ya nyuma katika uzinduzi rasmi wa Vodacom Miss Tanzania 2011
Baadhi ya kamati ya Vodacom Miss Tanzania walikuepo katika uzinduzi huo kulia ni Meneja udhamini wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Lino International Agency Hashimu Lundenga