b..

B1

Wynem

animation

Monday, January 24, 2011

MSHINDI MISS UTALII TANZANIA 2010- 2011 KUNYANYUKA NA SH. MILIONI MIA MOJA HAMSINI



Baadhi ya washiriki Miss Utalii Tz- 2010- 2011wakila tizi katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar, Jumapili
Washiriki Miss Utalii Tz- Kusini na Magharini kabla ya mchezo

Mbunge wa Kinondoni Idd Azan akisalimiana na washiriki wa Miss Utalii Tz Kaskazini wakati wa Mchezo wa Kirafiki Dhidi ya warembo wa Mashariki
Baadhi ya washiriki wa Miss Utalii Tz- 2010- 2011 katika mazoezi kabla ya Michezo ya wao kwa wao katika ufukwe wa Coco Beach
Juu na chini washiriki wa Miss Utalii Kanda ya Mashariki na Kaskazini wakichuana katika michezo ya Soka ya Ufukweni Coco Beach jana.
Wakati fainali za taifa za shindano la Miss Utalii Tanzania zimepangwa kufanyika usiku wa Februari 5, 2011, mrembo atakayenyakua taji la taifa la Miss Utalii mwaka huu ataondoka na faida kubwa ya zawadi ya mkataba wenye thamani ya shilingi milioni mia moja na hamsini.
Na Mwandishi wetu
Taarifa iliyotolewa na Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo imeeleza kuwa, shindano la mwaka huu litafanyika kwenye hoteli ya kitalii ya Kiromo View Resort iliyopo umbali wa kilometa kumi tu toka Bagamoyo mjini ambapo pia kutakuwa na burudani kadhaa zitakazosindikiza usiku huo adhimu na ya kihistoria katika tasnia nzima ya urembo na utalii hapa Tanzania.
Akaendelea kusema; washiriki wote wa fainali za Miss Utalii Tanzania 2010/11 wako katika hali nzuri kiafya na kisaikolojia kwa ajili ya shindano na kufafanua kuwa mbali ya kitita hicho kwa Malkia wa mwaka huu, warembo wengine wataweza kujitwalia mataji yatakayowakilisha hifadhi za taifa 16 zilizo chini ya mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kadhalika, Chipungahelo amesema kuwa mbali ya mataji ya hifadhi, pia, kutakuwa na tuzo zingine toka baadhi ya makampuni na taasisi zilizodhamini shindano hili ili kuyawakilisha katika suala zima la kuutangaza utalii kupitia hifadhi za taifa na utamaduni wa Mtanzania na hivyo kuongeza hamasa zaidi kwa washiriki ambao nao wameonesha kujawa shauku ya kufanya vema.
“Fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2010/11, zitakuwa tukio kubwa zaidi la kitaifa la kitamaduni na urembo nchini, ambalo kishindo chake kitaleta mageuzi makubwa katika sanaa ya urembo nchini, barani Afrika na duniani kwa ujumla. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa mara ya kwanza dunia itashuhudia idadi kubwa ya warembo wakiwa jukwaa moja wakitangaza na kuonesha utamaduni kupitia mavazi ya asili, ya kitalii, ya mitindo, ya ubunifu. Pia, warembo hao wataonesha vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za mikoa au kanda wanazowakilisha,’ amesema Rais wa Miss Utalii Tanzania.
Aidha, amewataja wadhamini wakuu wa shindano la taifa la Miss Utalii 2010/11 ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Business Times Limited, Kiromo View Resort na Sahara Media Group Limited,inayomiliki kituo cha runinga cha Star TV, Radio Free Africa, Kiss FM na gazeti la Msanii Afrika.Wengine ni Zizzou Fashion, Alaisy Travel, Auckland Tours, Tintona TankStation, Tesco Furniture, Mlonge By Makai Enterprises,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Coco Beach.
Warembo hao wameanza ziara rasmi za kutembelea na kutangaza vivutio vya utalii ,kwa kutembelea maeneo ya kihistoria yaliyopo Mkoani Pwani,ambapo juzi walitembelea Maeneo ya Kihistoria yaliyopo wilayani Bagamoyo ikiwemo Magofu ya Kaole,wakiongozwa na katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo.
Aidha jana warembo wote 60 walitembelea na kutangaza Fukwe za Bahari ya Hindi zilizoko mkoani Dar Es Salaam wakiongozwa na Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan. wakiwa katika Fukwe wa Coco Beach warembo hao wakiwa wamegawanywa katika timu nne za mpira wa miguu walishindana kusakata kabumbu la Ufukweni hali iliyopelekea kuwa kivutio kikubwa na kusababisha ufukwe huo kufurika mamia ya watu wakishuhudia warembo hao wakionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kandanda.
Michuano baina ya timu hizo za warembo zilizopewa majina ya hifadhi za Taifa ulikuwa mkubwa na kuamsha shangwe za mara kwa mara kwa wapenzi waliojazana kushuhudia mechi hizo. katika mchezo wa kwanza timu ya soka ya warembo wa Ngorongoro iliweza kuibwaga timu ya soka ya Selous kwa mabao 4-2 wakati katika mchezo wa pili ambao ulizikutanisha timu za Serengeti National Park dhidi ya Maunt Kilimanjaro na matokeo timu ya Mlima Kilimanjaro kuibuka kwa ushindi wa mabao 3-1.
Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan kwa kufurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na timu hizo za warembo wa miss Utalii Tanzania 2010- 2011 ambao tarehe 5 mwezi wa pili watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2010- 2011 katika Hotel ya Kitalii ya Kiromo Bagamoyo, alinunua kila goli kwa shilingi elfu kumi(10,000) hivyo aliweza kutoa shilingi laki moja kwa magoli kumi yaliyofungwa. naye mfanyabiashara maarufu nchini Zizzou Fashion alitoa seti nne za jezi kwa warembo wote 60

SAUTI ZA BUSARA AROUND DA CONER.


Djaaka was founded in Beira, Mozambique in 2001 by members from the big traditional music and dance company “Companhia de música e dança traditional da Beira”. Not long after their formation they won the regional young musicians’ festival Music Crossroads in 2002. It was here that they gained substantial regional exposure, winning several prizes, one of which was a visit to Fallun, the folk music festival in Sweden.

Their music reflects various traditions from central Mozambique. Djaaka’s sound can be identified largely by their use of marimba which comes from one area of central Mozambique called “Timbila” is heard on many of their songs. The music is contemporary with a strong traditional touch, both funky and deeply rooted. Djaaka sing in a dialect called Massena, which is not far removed from languages of Zambia, like Bemba and Njanja.

Djaaka is a true live band, skilled musician and good dancers, with outstanding outfits. Their live performance has impressed not only their home audience; it has brought them to festivals in Reunion, Mauritius, South Africa, Zimbabwe, Italy and United Kingdom. They have won the “best Mozambican band” award three times at TOP-Ngoma, held by Radio Mozambique.

Friday, January 21, 2011

KAKA ZAO KURUDI UPYA KWENYE GEMU


Kaka zao ni family inayotengenezwa na watu watano kutoka kanda ya ziwa mwanza. ambao ni Hardmad  mkushi a.k.a KIDUME akiwa kama kiongozi na Phantom ranks ambaye kwa sasa yuko nchini uswisi, wengine ni Fatma kilometa, Jahson pamoja na Susu.Tunafanya mziki aina ya dancehall na raga rumba.
Kwasasa makazi yetu ni hapa Dar es salaam kwa ajiri ya shughuli zetu za muziki.
Jahson ameachia Track pamoja na video inayoitwaHEAT akiwa na Hardmad na kwa sasa huko anafanya nyimbo nyingine inayoitwa SHOW ME SOME LOVEakiwa na Susu pamoja na Fatma. Hivi karibuni itakuwa hewani.
Big up sana kwa mashabiki wanaotupa suport pia big up kwa wapenzi wa dancehall pamoja sanaaaaaaaaaaaana
 R whu jah bless no man cian tes

Tuesday, January 18, 2011

CBH AACHIA NGOMA TATU KWA MPIGO.

Baada ku kutamba na vngoma ya ke ya Best Friend kwenye Oudio na Video msanii CBH watu walidhani amebahatika lakini kwa sasa anaonesha uwezo wake baada ya kuachia ngoma tatu kali zote zikiwa kwenye stail ileile kama aliyotoka nayo mwanzo. ngoma alizotoka nazo CBH ni
am in love, Broda na oweeeoh.
CBH kwa sasa anasimamiwa na kampuni ya muziki ya SHOW BIZ DIFINE chini ya mtu mzima Eyryn D.

Monday, January 17, 2011

BASATA LEO PALIKUWA HAPATOSHI

Katibu mtendaji wa baraza sanaa la taifa (BASATA) Ghonche Materego 
Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akiongea jambo kwenye jukwaa la sanaa
Hili ndio nyomi lililokuwepo pale kwenye jukwaa la sanaa kwenye ukumbi wa basata

Hawa ni baadhi ya wadau wakichangia mada iliyokwa ikizungumziwa.
Mrisho Mpoto akihojiwa na mwandishi wa habari mara baada ya kikao kuisha
Na hapa ni zamu ya Mkoloni kuhojiwa na mwandishi mara baada ya kikao kuisha

Sunday, January 16, 2011

MSIKILIZE NA MUONE MH. JOHN MNYIKA KATIKA KONGAMANO LA MCHAKATO WA KATIBA MPYA.

GAZETI LAKO LA DIRA LIPO MITAANI TENA LEO.


Kama kawaida gazeti lako la DIRA lipo miataani leo hii likiwa limesheheni habari zilizofanyiwa uchunguzi na kuhakikiwa kwa umakini kabia. linapatikana kwa Tsh. 500/= tu. Pata kopi yako mapema usikubali kuukosa uhondo huu.

BENJAMINI WA MAMBOJAMBO BADO YUKO CHIMBO.

Leo nimepokea meseji kutoka kwa kaka bjamini wa mammbojambo akisema kwamba wadau wasimuone kama kakaa kimya sana ila ni kwa sababu yuko chimbo anaandaa albamu.mesji ilkua hivi......
"mambo vipi kaka a.k.a Mtoto wa kitaa! naomba unisaaidie kuwaambia mafans wangu kuwa wasijali na wala wasiogope kwa mimi kukaa kimya, sasa hivi nipo chimbo naandaa ngoma kalikali ambazo zitawarusha kiuhakika,pia ndio naandaa albam yangu ambayo nategemea kuiachia kitaani mwezi mei, na cha mwisho napenda kuwaambia mashabiki na wapenzi wa muziki wangu kuwa bado nipo nao kwa kila kitu kwani Benjamini ni yuleyule wa siku zote ambae anawapa vitu vikali siku zote."
Mesiji iliishia hapo. Sule's Inc. & entertainment  inamtakia Benjamini Mafanikio mema katika harakati za kuupeleka huu muziki wetu mbele. 2PO PA1

Thursday, January 13, 2011

USIKU WA BEN POUL WITH THE M BAND LEO


WELCOME TO THE MUSIC NIGHT WITH THE M BAND EVERY THURSDAY @BUDHABLU LOUNGE MIKOCHENI NEAR DR. KAIRUKI'S HOSPITAL, FROM 8:00pm TILL 00:00pm, THIS THURSDAY BEN POL WILL BE PERFORMING LIVE WITH THE M BAND, Tsh. 5000 @ THE GATE.

BASATA YAUKARIBISHA MWAKA KWA KISHINDO KATIKA SEKTA YA SANAA

Afisa wa Sanaa za Maonyesho kutoka BASATA Rajab Zubwa (Kulia) akilicharaza gitaa huku Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi (Kushoto) na Katibu wake wakisakata
Baadhi ya wafanyakazi wa BASATA wakiinamisha vichwa kwa dakika moja kwenye hafla ya kuukaribisha mwaka 2011 kama ishara ya kuwakumbuka wasanii na wadau wa sanaa waliotutoka katika kipindi cha mwaka wa 2010.
Wafanyakazi wa BASATA pamoja na baadhi ya wageni waarikwa wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kupata maakuli.
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa BASATA wakiyarudi magoma.Hakika ilikuwa ni furaha.

Na Mwandishi Wetu

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wiki hii limefanya hafla fupi ya kuukaribisha mwaka huku Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Ghonche Materego akiwatangazia wafanyakazi kwamba,mwaka huu wa 2011 ni wa kazi na kasi kubwa katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya sanaa.
Materego alianika mikakati iliyopo kuwa ni pamoja na kuhakikisha ukumbi mkubwa wa burudani wenye uwezo wa kuchukua watu 1,000 unakamilika, tamasha kubwa la siku ya msanii wa Tanzania linafanyika kwa mafanikio makubwa, mashirikisho ya sanaa nchini yanafanya kazi kwa ufanisi na kiwango cha juu na mikakati mingine mingi.
“Mwaka huu lazima tufanye kazi kwa kasi na kiwango kikubwa,lazima ukumbi wetu wa BASATA umalizike kwa hali na mali,tamasha kubwa la msanii wa Tanzania lifanyike kwa mafanikio.Ni mwaka wa kuleta mabadiliko kwenye sekta yetu ya sanaa” alisisitiza Materego.
Aliwaasa viongozi wa mashirikisho ya sanaa nchini waliohudhuria hafla hiyo kwa niaba ya wasanii wote nchini kwamba, lazima wahakikishe wanawaunganisha wasanii katika kupigania maslahi na hki zao na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea lakini kubwa kuhakikisha mchango na takwimu sahihi za sekta ya sanaa zinapatikana.
Akiongeza zaidi alisema “Changamoto tuliyonayo mbele ni ya kuwa na takwimu sahihi katika sekta yetu ya sanaa.Kwa muda mrefu sekta yetu imekuwa ikifichwa kwenye sekta nyingine hivyo mchango wake kwenye pato la taifa kutokutambuliwa moja kwa moja.Ni wajibu wetu sasa kuhakikisha tunakuwa na takwimu sahihi za sekta hii.
Hafla hiyo fupi ya BASATA ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2011 ilifanyika kwenye viwanja vya baraza hilo na kuhudhuriwa na wafanyakazi wote,viongozi wa mashirikisho ya sanaa nchini na uongozi wa juu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Burudani.

Monday, January 10, 2011

WADAU MSAADA WENU UNAHITAJIKA KWA KIASI KIKUBWA.

Tuombe msaada kuwasaidia wenzetu ambao ni
mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu...

Ninakuomba kama mtanzania mwenzangu tupeane hamasa ya kupendana na kusaidiana sio katika sherehe za starehe tuu, zaidi siku hizi tuzidishe kusaidiana katika shida maana sasa shida zinazidi siku hadi siku.
Katika pitapita zangu, nimekutana na mtoto huyu Abdully mwenye ulemavu wa viungo huko Kaole, Bagamoyo. Kula kwake kwa taabu, haongei, ingawa anacheka akifurahishwa, na kulia kwa kupiga kelele akiudhiwa au akiwa na maumivu ingawa hawezi kuelekeza maumivi yako wapi.
Cha kusikitisha, mama yake mzazi amemkimbia mtoto na mume, baba nae ameanza kukata tamaa ya mwanae kwa kukosa muelekeo na msaada (support). Baba (Bw. Hamoud) anaishi na mama yake mzazi ambaye ni mtu mzima mwenye matatizo ya kiafya, macho na thyrod eshafanyiwa upasuaji nk... sasa Bw Hamoud ameacha shughuli za kutafuta fedha za kukimu maisha ili aweze kumlea kijana Abdul (4) ananza asubuhi kwa kumuosha, kumlisha kifungua kinywa..... mchana kumlisha anakula kwa taabu maana ulimi hauzunguki sawa sawa kama vile umepooza, na koo halimezi vizuri.... jioni anamsafisha na kumlisha.... maisha yamekuwa duni, kwa hivyo hata malezi ya Abdul yamekuwa magumu mno...
Alishauriwa ampeleke hospitali ya CCBRT, nae baada ya kwenda hapo alishauriwa ampeleke kwa physiotherapy kila wiki, tatizo la Bw Hamoud ni usafiri kutoka Kaole hadi msasani CCBRT ni wa daladala na mtoto mwenye ulemavu wa viuongo si mchezo... mlemavu wa aina hii anaweza kuwa na haja kubwa au ndogo mahali popote wakati wowote hata mkiwa ndani ya daladala huduma yake ngumu hapo ni mtihani...

Hapo CCBRT wanaweza kushinda kutwa kabla ya kupata huduma kipindi hicho cha kusubiri mtoto amebebwa au kupakatwa, chakula hakuna, na pahala pa kumlaza aweze anaglau kunyoosha viuongo hakuna. wahudumu wanapita na kumuangalia hapo katika foleni bila kumpa tamaa au hata nasaha. Jioni usafiri wa wa kubanana ndani ya daladala kurudi Bagamoyo, pikipiki hadi Kaole.... Baba Abdul kaishiwa nguvu ameshindwa. Wapo Kaole wanasubiri hatma ya Mwenyezi Mungu.
Abdul amepewa ki "baiskeli" cha mtoto (push chair) na akiwekwa hapo lazima afungwe na khanga ndio akae kwa usalama na kwa sasa anabanwa hapo....

Hivyo basi Kama kuna wasamaria
wenye huruma na hali hii, wanaomba:

1. Wheelchair ya kawaida Abdul akae
kwa usalama na awe na nafasi viungo viwe huru
2. Ushauri kwa kiafya
3. Ushauri wowote, na msaada wowote
utakaoweza kutoa afueni kwa Abdul na baba yake Hamoud

mpigie simu Hamoud
+255 757 652449 na +255 787 771566
kwa msaada au ushauri. Juhudi za kufungua
akaunti maalumu zinafanywa kwa wenye
kutaka kumsaidia mtoto Abdully
Mdau Dar

Sunday, January 9, 2011

FACEBOOK WILL END ON MARCH 15th!



PALO ALTO, CA –Mark Zuckerberg announced that Facebook will be shut down in March. Managing the site has become too stressful.

“Facebook has gotten out of control,” said Zuckerberg in a press conference outside his Palo Alto office, “and the stress of managing this company has ruined my life. I need to put an end to all the madness.”
Zuckerberg went on to explain that starting March 15th, users will no longer be able to access their Facebook accounts.
“After March 15th the whole website shuts down,” said Avrat Humarthi, Vice President of Technical Affairs at Facebook. “So if you ever want to see your pictures again, I recommend you take them off the internet. You won’t be able to get them back once Facebook goes out of business.”
Zuckerberg said that the decision to shut down Facebook was difficult, but that he does not think people will be upset.
“I personally don’t think it’s a big deal,” he said in a private phone interview. “And to be honest, I think it’s for the better. Without Facebook, people will have to go outside and make real friends. That’s always a good thing.”

Some Facebook users were furious upon hearing the shocking news.

“What am I going to do without Facebook?” said Denise Bradshaw, a high school student from Indiana. “My life revolves around it. I’m on Facebook at least 10 hours a day. Now what am I going to do with all that free time?”
However, parents across the country have been experiencing a long anticipated sense of relief.“I’m glad the Facebook nightmare is over,” said Jon Guttari, a single parent from Detroit. “Now my teenager’s face won’t be glued to a computer screen all day. Maybe I can even have a conversation with her.”Those in the financial circuit are criticizing Zuckerberg for walking away from a multibillion dollar franchise. Facebook is currently ranked as one of the wealthiest businesses in the world, with economists estimating its value at around 7.9 billion.But Zuckerberg remains unruffled by these accusations. He says he will stand by his decision to give Facebook the axe.
“I don’t care about the money,” said Zuckerberg. “I just want my old life back.”
The Facebook Corporation suggests that users remove all of their personal information from the website before March 15th. After that date, all photos, notes, links, and videos will be permanently erased.

DIRA LIMEFUNGUKA TENA KAMA KAWAIDA YAKE. LIPO MTAANI LEO. PATA NAKALA YAKO.

Kama kawaida gazeti lako la Dira ya mtanzania  linalotolewwa na Dira Media Group lipo mtaani leo hii likiwa na habari kemkem za kiuchunguzi na zilizohakikiwa kwa umakini zaidi. pata nakala yako sasa ili ujionee mwenyewe. 

Wednesday, January 5, 2011

CHADEMA WACHEZEA KICHAPO BAADA YA KUKAIDI AGIZO LA POLISI


Mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa, Josephine akiwa ametapakaa damu baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kipigo na polisi wakati wakivunja maandamano ya viongozi na wanachama wa chama hicho yaliyofanyika mjini Arusha jana.Katika maandamano hayo watu kadhaa walijeruhiwa baada ya kupigwa na pilisi wa kutuliza ghasia.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, wakiongowa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe (Watano kulia) na katibu mku, Dk.Wilbroad Slaa(Wasita kulia) wakiongoza maandamano yaliopigwa marufuku na polisi jana mjini Arusha.Hatimaye polisi iliwatolea uvivu na kuwapiga kwa mabomu ya machozi. Habari zaidi zaeleza kuwa Mbowe anashikiliwa na polisi.
Askari Polisi wakijaribu kulizuia gari moja lilikuwepo katika maandamano hayo.
Wanausalama wakimtuliza mmoja wa waandamanaji aliekuwepo katika maandamano hayo.
Wakazi wa maeneo ya jirani na zilipotokea vurugu hizo wakinawa maji usoni ili kupunguza makali ya sumu za mabomu ya machozi yaliyokuwa yakilipuliwa katika kutuliza ghasia hizo.
Mitaa ya Jijini Arusha ililindima milio ya Mabomu ya Machozi huku mitaa ikiwa imepoa kabisa.
Askari Polisi wakiwa wameenea kila kona kuhakikisha hali inakuwa shwari na hakuna mtu anaefanya maandamano hayo

Tuesday, January 4, 2011

MC GEORGE AANZA KWA KUSIMULIA HADITHI.

Mtu mzima George Mc ameamua kuingia studio na kudhiirisha kua anauwezo wa kufanya muziki na ukaeleweka. George ambae ameachia video yake ya kwanza kabisa alaiyoipa jina la HADITHI akiwa ameifanyia katika studio za 24/7 chini ya mtayarishaji Vill, Pia Georhe amesema tusubiri mambo mazuri mengi kutoka kwake kwani amejipanga na ana madini na silaha za kutosha za kutosha kabisa.

BASATA KUJA NA TAMASHA LA SIKU YA MSANII WA TANZANIA

Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego (Kushoto) akisisitiza jambo wakati akichangia kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa BASATA.Kushoto kwake ni aliyekuwa Mratibu Msaidizi wa Tamasha la Sauti za Busara,Kwame Mchauru na Katibu wa CAJAtz,Hassan Bumbuli.

Na Mwandishi Wetu

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) baadaye mwaka huu litaandaa tamasha kubwa la wasanii ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka likiwa na jina la siku ya msanii wa Tanzania.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika katika ukumbi wa baraza hilo kila Jumatatu,Katibu Mtendaji wake Ghonche Materego alisema kwamba,tamasha hilo ambalo litakuwa likipambwa na burudani kemkem kutoka kwa wasanii wa sanaa mbalimbali hapa nchini litakuwa ni maalum kwa ajili ya kuenzi sanaa na kusisitiza kaulimbiu ya sanaa ni kazi kwa vitendo.

“Katika kuhakikisha sanaa inakuwa kweli kazi na ajira kama ilivyo kaulimbiu yetu mwaka huu,watendaji wa BASATA wako katika maandalizi ya kuandaa tamasha la siku ya wasanii ambalo tutawapa taarifa zake hivi karibuni.Katika tamasha hilo wasanii wetu watapata fursa za kuonyesha kazi zao na kushiriki kikamilifu” alisema Materego.

Aliongeza kwamba,tamasha hilo litakuwa ni mwanzo wa kuenzi wasanii wetu na kukuza sekta ya sanaa nchini hasa ikizingatiwa itakuwa ni fursa kwa wasanii kujitangaza na kupanua mwanya wa masoko ya kazi zao.

Huku akiomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa wadau mbalimbali hasa wale wa sanaa,Materego aliongeza “Tunataka wasanii wetu sasa waone faida ya kazi zao,wazalishe sanaa zenye ubora na zinazoweza kukubalika na kuvuta watu wengi.Hii ndiyo siri pekee ya kuwafanya wapate fursa ya kushiriki maonyesho na matamasha mbalimbali ya sanaa ndani na nje ya nchi lakini pia kufanya kazi zao ziuzike”.

Awali akiwasilisha mada katika Jukwaa la Sanaa,iliyohusu Mchango wa Matamasha ya Sanaa Katika Kukuza Ajira nchini Tanzania,aliyekuwa Mratibu Msaidizi wa onyesho maarufu hapa nchini la Sauti za Busara,Kwame Mchauru alisema kwamba, wasanii hawana budi kutengeneza sanaa zenye ubora na zenye asili ya Tanzania ili kuweza kupata fursa ya kushiriki maonyesho na matamasha mbalimbali ya ndani na nje ya nchini.

Aliongeza kwamba, matamasha na maonyesho ya kazi za sanaa ndiyo daraja kubwa la mafanikio kwa wasanii hivyo hawana budi kusaka fursa za kushiriki kikamilifu na kuhakikisha kazi zao zinakuwa na ubora unaohitajika kwani hicho ndicho kigezo kikubwa cha kuwawezesha kushiriki

Monday, January 3, 2011

KAA TAYARI KWA YOUNG VJ KUTOKA KIJENGE JUU.

YOUNG VJ Mwana hiphop anaechipukia kwa kasi kutoka ARA Chuga akiwa katika pozi tofauti tofauti

Meseji niliyoipokea kutoka kwa YOUNG VJ imeandikwa hivi 

".........Mambo vipi kaka Sule a.k.a mtoto wa kitaa naomba uwape habari wadau wangu na wapenzi wote wa burudani kuwa Mikakati yangu ya mwaka huu mpya ni kuleta vi2 vipya  so wapenzi  wangu na wapenzi wa hiphop  wakae  mkao wa kula Kwani  muda si mrefu ntaachia nyimbo mpya  ambayo naamini   itantambulisha vizur ktk ulimwengu  wa bongo fleva.

..........Pia  namshkuru  mungu sana coz napata sapoti kubwa kutoka kwa kaka  zangu wakaribu JCB wa WAtengwa  na DX wa NOIZMEKAH na kuhusu  ushindani wa  game la leo  haswa kwa  wanamuziki  wadogo kama mimi, Young Dee na Dogo Janja. mimi kama mimi nawaachia  mashabiki  kwan  wao ndio wataamua nani wa kumpa ubingwa kutokana na mpambano wa gem lenyewe"

YOUNG VJ alimalizia kwa kusema "kaka mimi nakutakia heri na baraka na mafanikio katika maisha kwani unafanya kazi nzuri katika kutupa habari nzuri na zenye uhakika. siku njema"