Mbunge wa viti maalum Mary Chatanda akisalimia katika kikao cha baraza kuu la UWT mkoa wa Iringa |
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akifungua baraza kuu la UWT mkoa wa Iringa |
Wajumbe wa baraza kuu ya UWT mkoa wa Iringa |
Msambatavangu akiagana na wajumbe wa baraza kuu la UWT mkoa wa Iringa kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini , mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na Rose Tweve |
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu wa tatu kushoto akiwa na viongozi mbali mbali wa mkoa |
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi akitoa salam za utangulizi |
Na matukiodaimaBlog
BARAZA kuu la umoja wa wanawake mkoa wa Iringa limempongeza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kwa kuwa kiongozi wa mfano ndani ya mkoa na nje ya mkoa wa Iringa na hivyo kumwomba kugombea tena nafasi hiyo ya uenyekiti mwakani 2017.
Akitoa pongezi hizo leo wakati akishukuru kwa niaba ya wajumbe wa baraza kuu la UWT mkoa lililokutana kwenye ukumbi wa CCM wilaya ya Iringa mjini ,mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini ambae pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) alisema kuwa ushindi mkubwa ambao CCM iliupata katika uchaguzi mkuu mwaka jana uchaguzi uliomwezesha Rais Dkt John Magufuli kushinda kwa kishindo dhidi ya wapinzani wake ni pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Msambatavangu katika kampeni za uchaguzi mkuu .
Mkini alisema mkoa wa Iringa kwenye uchaguzi huo uliweza kufanya vizuri kwa kushinda majimbo 6 kata ya 7 yaliyopo ndani ya mkoa wa Iringa na kuwa pamoja na kila mmoja kushiriki katika kupigania ushindi huo wa chama ila wao kama wanawake hawanabudi kumpongeza mwanamke mwenzao ambae ndie mwenyekiti wa chama mkoa kwa kuonyesha Taifa kuwa wanawake wanauwezo wa kuongoza .
'' Naomba kuchukua nafasi hii kwa niaba ya wanawake wenzangu kukupongeza sana mwenyekiti wetu wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu umeonyesha mfano mzuri kuwa unaweza kuongoza .......nakumbuka wakati wa kampeni wewe ulisimama kidete kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo mbali ya figisu figisu zilizokuwa zikielekezwa kwao ila hukuteteleka ''
Mbali ya mwenyekiti kufanya vema katika kampeni za 2015 ila hajaacha kuitumikia vema jamii ya mkoa wa Iringa ikumbukwe mkoa umepata misiba miwili mikubwa ukiwemo wa aliyekuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa Tasili Mgoda na mwasisi wa maendeleo ya wilaya ya Mufindi Joseph Mungai shughuli zote zimeratibiwa vema na Msambatavangu tena pasipo ubaguzi wowote .
'' Mwenyekiti wetu anafanya kazi vizuri ndani ya mkoa wetu tena pasipo ubaguzi wowote na ni mtetezi mzuri sana kwa wanawake ndani ya mkoa na hanaga unafiki kabisa kwani yeye siku zote husema kweli tupu ''
Mkini alisema kuwa kutokana na utendaji kazi wake mzuri ndani ya chama wao wanaona bado mwenyekiti huyo anauwezo wa kuwavusha wana CCM kwa miaka mingine mitano ijayo hivyo kumshawishi kuingia tena ulingoni mwakani 2017 katika uchaguzi mkuu wa viongozi ngazi mbali mbali za chama.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi akisoma tamko la UWT mkoa wa Iringa kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt Magufuli alisema kuwa wao kama wanawake wa CCM wameendelea kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt Magufuli na kuwa kubwa zaidi ni jinsi Rais alivyoweza kujibu maswali ya watanzania kupitia mkutano wake wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini.
.Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa ,Msambatavangu pamoja na kupongeza pongezi za baraza hilo dhidi yake na zile za Rais alisema atahakikisha pongezi za wanawake hao zinamfikia Rais Dkt Magufuli huku akisisitiza wanawake kuendelea kuongoza nafasi zao kwa kujiamini zaidi badala ya kutanguliza uoga usio wa lazima .
Alisema wakati chama kinajiandaa kwa chaguzi zake mwakani ni vizuri wanawake kuanza kujipima ama kuwapima wale ambao wanaingia kuwania nafasi mbali mbali ili kupata viongozi wenye uwezo wa kuwatumikia wananchi hasa katika kipindi hichi cha kujenga chama chenye nguvu na uongozi wenye uwezo wa kuendana na kauli mbiu ya Rais ya hapa Kazi tu.
Kwani alisema wapo baadhi ya watu ndani ya CCM kazi yao ni kusubiri uchaguzi hadi uchaguzi kufanya kazi za chama na kuwa wanachama hao hawapo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi bali wapo kwa ajili ya kutumikia matumbo yao jambo ambalo halikubaliki kwa uhai na nguvu ya CCM .
Mwenyekiti huyo alisema hivi sasa wananchi wanauelewa mkubwa juu ya siasa na uongozi hivyo ni lazima wanaopewa nafasi za kugombea ni lazima wawe wanakubalika katika jamii inayowazunguka vinginevyo chama kinaweza kuyumba iwapo watu wasio na sifa watapewa nafasi za kugombea hivyo ni vizuri kuanza kuwatafuta watu wanaofaa ambao hawapo ndani ya CCM kujiunga na CCM ili mbeleni waje kugombea kupitia CCM.
Kwani alisema hivi sasa kote duniani ni vema viwili pekee ndivyo vimebaki kuitwa vyama tawala na vyama hivyo ni nchini China na Tanzania pekee ila maeneo mengine yote vyama tawala imeondolewa madarakani kwa kuwa CCM lengo lake ni kuendelea kuongoza ni vizuri kila mwanachama na kila kiongozi kuhakikisha anawajibika vema kwa wananchi kama ambavyo mwenyekiti wa chama Taifa Rais Dkt Magufuli anavyoliongoza Taifa kwa faida ya watanzania na vizazi vijavyo.
No comments:
Post a Comment