Mwandishi Wetu
Chama cha watanzania waliosoma China- CHINA
ALLUMNI ASSOCIATION OF TANZANIA (CAAT) hii leo tarehe 27 August, 2016
kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wake wapya.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika katika
ukumbi wa Rombo Green views Hotel sinza Dar es salaam kuanzia saa saba kamili
mchana nakufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza viongozi wapya na kuwaaga viongozi
waliomaliza muda wao.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa uchaguzi wa chama
hicho GUSTAV SANGA uchaguzi huo utawaweka madarakani viongozi hao miaka mitatu
kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni
Chairperson, Secretary, Treasurer, Director of Statistics, media and
information, director of Art, culture and heritage pamoja na Director of
Education, Science and Technology
SANGA pia amewakaribisha watanzania wote
waliomaliza China kujiunga katika chama hicho ili kuweza kutimiza malengo
mbalimbali waliyojiwekea ikiwemo kuishauri serikali masuala yahusuyo TANZANIA-
CHINA.
Chama hicho cha watanzania waliosoma China
kina miaka sita tangu kuanzishwa kwake na kina wanachama tangu waliosoma china
miaka ya1980 kwa ngazi ya shahada , astashahada na shahada ya uzamivu.
No comments:
Post a Comment