b..

B1

Wynem

animation

Wednesday, April 2, 2014

HIZI NDIO PICHA ZA KINA KOLO NA MUSTAPHA ZILISABABISHA MSANII NYOTA NDOGO KUANDAMANA

Screen Shot 2014-03-25 at 1.29.26 AM
Colonel Mustapha ni miongoni mwa Wasanii wa longtime kidogo kwenye game ya muziki Kenya toka enzi hizo akiwa kwenye kundi lililotoa hit single yenye maneno ‘bibi yake mufupi, kijana murefu ametoka wapi’
Hivi karibuni ameingia kwenye vichwa vya habari sana hasa baada ya kutangaza kuwa mapenzini na Huddah, mrembo aliewahi kuiwakilisha Kenya kwenye shindano la Big brother Africa ambapo uhusiano wao hauchukua muda mrefu ukavunjika.
Kabla ya kuvunjika, tayari walikua wameshapiga picha ambapo Mustapha anasema alikua amerekodi wimbo na Huddah lakini walipoachana mrembo huyu akasema Ogopa Dj’s wasiitumie tena sauti yake kwenye huo wimbo na kama watafanya hivyo atawashitaki.
Hata hivyo picha zao wawili zilishasambaa kwenye internet tayari na kuanza kuchukua headlines kutokana na pozi zao.

Screen Shot 2014-03-25 at 1.29.51 AM
Kuonyesha kupinga hiki kitendo, mwimbaji staa wa ‘watu na viatu’ Nyota ndogo aliungana na Wanawake wengine Mombasa na kuandamana kupinga kitendo cha Mustapha kuzisambaza picha zinazomdhalilisha Mwanamke hivyo aombe msamaha haraka iwezekanavyo.
Screen Shot 2014-03-25 at 1.30.18 AM
Namkariri Nyota akisema ‘Mustapha ambae ni msanii mkubwa ameanza muziki kitambo kuchukua picha za watoto wa kike na kuwavua nguo, hii itanyima hata Wazazi kuachia watoto wao kufanya muziki unaoonekana uhuni… ikiwa Mustapha hatoacha hii itatuharibia, kama kaona ameshindwa kutunga nyimbo zitazowashika watoto wa sasa hivi afate mtoto amuandikie’
‘Ameona jina linashuka ndio maana bora achukue picha za uchi atengeneze skendo, Mustapha nimekua nae kwenye muziki miaka mingi, kwa nini sasa hivi ndio afanye kwa sababu Prezzo anafanya? ama ameona Prezzo yuko juu kwa sababu anafanya.. yeye ndio anatakiwa kumwambia Prezzo usifanye hivi’

Screen Shot 2014-03-25 at 1.34.45 AMScreen Shot 2014-03-25 at 1.35.12 AM
Hata hivyo Mustapha amezungumza baada ya haya maandamano na kusema ‘Ni kitu cha kushtua kuona maandamano yamefanyika kwa ajili ya Mustapha, wakati tunapiga hizi picha hakukua na lengo lolote la kumdhalilisha Mwanamke bali ilikua mambo yetu yenyewe kwa raha zetu, nilivyoona youtube kuhusu haya maandamano nimehuzunika… naomba msamaha kwa yeyote aliekerwa na hili… nimekubali kuomba msamaha kwa Wanawake’
Kwa kumalizia Mustapha amesema ‘kuna Wasichana ambao wanataka tupige hizo picha na wananilipa’

Screen Shot 2014-03-25 at 1.37.19 AM

No comments:

Post a Comment