Na Andrew Chale, Zanzibar.
MWANAMUZIKI
nguli wa miondoko ya Afro rege, Jhikoman Manyika jana usiku Februari
13, aliwasha moto kwa kupiga shoo ya nguvu iliyodumu kwa lisaa limoja
na kukonga nyoyo umati mkubwa uliojitokeza kwenye tamasha hilo la 11,la
Sauti za Busara mwaka huu 2014. Jhikoman alipanda jukwaani majira ya saa
tatu usiku sambamba na bendi yake ya Afikabisa na kupiga vionjo
mbalimbali vya nyimbo zake za sasa na za nyuma.
Jhikoman
aliweza kuwasha moto huo kwa kupiga nyimbo zake zilizopo kwenye albamu
yake ya Chikonda na nyingine hali iliyokonga wadau hao wa muziki
wakiwemo wageni kutoka mataifa mbalimbali na watanzania waliojumukika
kwenye tamasha hilo.
Hata
hivyo, Jhikoman alisema baada ya shoo hiyo anatarajia kupiga shoo
zingine kwenye nchi mbalimbali kwa kufanya ziara maalum ikiwemo mataifa
ya Ulaya. Mbali na Jhikoman wasanii wengine ni pmoja na kundi la Seven
Survivor wanopiga muziki wa mchiriku, huku kundi la Baladna taarabu wao
walikonga nyoyo kwa muziki wa mwambao na taarabu asili. Wengine ni kundi
la Pongwa kutoka visiwani Zanzibar, Tritonik (Motius), na nyingine
nyingi.
Awali
tamasha hilo lilifunguliwa kwa paredi iliyokusanya wanamuziki mbalimbali
kutoka mataifa yote na kwa kila mmoja kuonyesha muziki wake mitaani na
kasha kumalizikia kwenye viunga vya Ngome Kongwe. Aidha
tamasha hilo la siku nne, linatarajiwa kuwa na wanamuziki mbalimbali
vikiwemo vikundi 32, vyenye jumla ya wasanii 200, ambao watapiga shoo
kwenye jukwaa hilo la Kimataifa. Hadi sasa mji wa Zanzibr umebarikiwa
kuwa na wageni mbalimbali wakiwemo waliofika maalum kwa ajili ya shoo na
wale wanaokuja kupumzika kwenye kisiwa hiki cha marashi ya
karafuu.Aidha, tayari idadi ya wageni imeongezeka huku baadhi ya hoteli
zikiwa zimefurika na biashara za kitalii zikiwa zinanunuliwa kwa
wingi.
Kwa
upande wake, David Ojoy ambaye ni msaidizi wa masuala ya habari wa
tamasha hilo, anasema kuwa hali ya wageni imekuwa kubwa kufika kwenye
tamasha hilo ikiwemo kupata habari mbali mbali zinazoptikana kwenye
mtandao maalum wa tamasha hilo pamoja vyombo vya habari. "Tunavipongeza
vyombo vya habari kwa kutupa sapoti na tunaomba tuendelee hivyo hivyo
ilikukuza muziki wetu wa kiafrika na kujenga tamaduni imara hapa afrika
na tamasha hili liendelee kuwa la kimataifa zaidi" alisema Ojay.
No comments:
Post a Comment