Asia dachi ambae ndiye mwanamitindo anaeshikilia taji hilo baada kuvikwa mwaka 2010 ametoa wito kwa wasichana wenye vipaji vya uanamitindo kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili hii kwaajili ya usaili wa kujiunga na shindano hilo.
Pia nawaomba wabunifu wa mitindo ya nguo kujitokeza kuwavalisha wanamitindo watakaokuwa wamechaguliwa kwani kwakufanya hivyo mtapata nafasi ya kujitangaza na kuunga mkono harakati za ukuaji wa sanaa ya mitindo nchini Tanzania. Ushirikiano mzuri umeonyeshwa na wabunifu nguli Asia Idarus na Gabriel Molel kwa kujitokeza na kuunga mkono harakati hizi za unique model 2012 ambapo inategemewa kuwa chombo pekee cha kukuza sanaa ya wanamitindo wachanga nchini Tanzania. Usaili huo utafanyika tarehe 18 novemba katika hoteli ya Lamada iliyopo msimbazi center kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa saba mchana.
No comments:
Post a Comment