Saturday, January 10, 2015
PICHA ZA MDAU, SULE JUNIOR (MTOTO WA KITAA) AUAGA UKAPERA
Monday, December 22, 2014
BONDIA TWAHA KASSIM WA MOROGORO AMTWANGA KWA KO, MUSSA CHITEPETE WA SONGEA
Mabondia Twaha Kassim wa morogoro kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mussa Chitepete wa Songea wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kassim alishinda kwa K,O ya raundi ya sita
Bondia Mussa Chitepete wa Songea akiwa chini baada ya kupokea konde zito kutoka kwa Twaha Kassimu wa Morogoro wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kassim alishinda kwa K,O ya raundi ya 6
Bondia Cosmas Cheka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ramadhani Shauri wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Cheka alishinda kwa point mpambano uho wa raundi 8.
Picha Zote na SUPER D BOXING NEWS
Sunday, December 21, 2014
NGOMA MPYA YA MOPLUS - WAFUNDISHE
Bofya HAPA https://mkito.com/song/wafundishe/7941 kupakua wimbo wa Moplus aka Baba Wa Ukoo Kwa jina "WAFUNDISHE",ikiwa ni HipHop category
NGUNI KUPIGWA JANUARY 2 IFAKALA UKUMBI WA MAKUTANO IFAKARA

Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa ngumi wa kufungua mwaka unatarajia kupigwa Ifakala mkoa wa morogoro kwa ajili yas kuhamasisha na kukuza mchezo wa masumbwi nchini akizungumza na waandishi wa habari promota wa mpambano huo, Hiari Bohari amesema kuwa kwa sasa anataka aendereza mchezo wa masumbwi Ifakala kwa kuwa watu wapo na mchezo unapendwa
aliongeza kwa kusema siku hiyo ya january mbili itakuwa ni siku ya kufungua mwaka kwa mpambano wa masumbwi kati ya Abdallah Kilima na Abdul Amwenye uku Saleh Makuka akipambanma na Said Chamak
vile vile kutakuwa na mpambano miwili kwa ajili ya kuamasisha wanawake waje washiriki katika michezi ya ngumi siku hiyo Aika Georger atapambana na Najma Ally
aliongeza kwa kusema anawaomba wadau mbalimbali kutoa sapoti na kumuunga mkono katika harakati za kuinua mchezo wa masumbwi ili uweze kusonga mbele
Friday, December 19, 2014
STEPS KUTAMBULISHA FILAMU KATIKA MUONEKANO MPYA KWA MWAKA 2015
Mratibu wa mpango mpya wa Steps Entertainment, myovela Mfwaisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji na mwongozaji wa Filamu nchini, Jackob Steven 'JB' akizungumzia ujio mpya wa Steps.
Wakionesha Makasha mapya ya muvi za kibongo zitakazoanza kusambazwa na Steps mwaka 2015
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya usambazaji wa filamu bora Tanzania ya Steps Entertainment Ltd inatarajia kutoa bidhaa mpya za filamu kwa mwaka ujao wa 2015 filamu zenye ubora muonekano mzuri huku pia kuwaletea walaji bei rafiki kutoka kampuni bor a ya usambazaji wa filamu Tanzania Steps Entertainment Ltd.
Steps Entertaiment Ltd ni ilioanzishwa mwaka 2007 nchini Tanzania na makao yake makuu yako jijini Dar salaam, Kampuni ya Steps Entertainment inajishughulisha na usambazaji wa filamu za Kitanzania maarufu kwa jina la BONGO MOVIES
Tangu kuanzishwa kwake Kampuni ya Steps Entertainment imekuwa mdau mkubwa katika kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania na mpaka sasa ndiyo kampuni kubwa ya usambazaji wa filamu nchini Tanzania.
Kampuni ya Steps Entertainment kupitia mikakati yake ya kuinua tasnia ya filamu nchini Tanzaania imefanikiwa kutoa ajira nyingi kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu, wakiwemo waandaaji wa filamu, Waigizaji, Wasambazaji wakubwa kwa wadogo, Wauzaji wa rejareja na wanaoonyesha na au kukodisha katika vibanda.
Akiongea na wanahabari Carlos Johns Silondwa mtendaji mkuu ameielezea Steps Entertainment imefanikiwa pia kuvuka mipaka na kufikisha sinema za kitanzania katika mataifa mbalimbali ya nje na katika luninga za kimataifa na televisheni za ndani kuonyesha kazi za nyumbani.
“Kwa sasa mataifa mengi Ulaya na nchi za Scandinavia wanajifunza Lugha yetu ya Kiswahili kupitia filamu zetu, moja kwa moja utaona njia nyingine katika kukuza Kiswahili nje ya nchi kwa njia ya filamu tu ambazo zinasambazwa na kampuni hii, na kutengeneza ajira kwa vijana wengi,”
Pia kampuni imekuja na bei rafiki kwa mlaji baada ya kilio chake kuumiza kwa muda mrefu, kampuni kwa kutumia wataalamu pamoja na wadau wa filamu kutoka sehemu mbalimbali wamefanya utafiti ili kupata Mwarobaini wa Maharamia wa kazi za nyumbani kampuni imeshusha bei.
Hiyo inatokana na hali halisi filamu inatakiwa imfikie mtumia kwa 6,000/ lakini utafiti umebaini kuwa mtanzania anatumia zaidi kiasi cha 34,000/ na zaidi bila kuimiliki Dvd hiyo, baada ya Vibanda au Library kuanzimisha, badala ya kumuuzia.
Filamu ambayo itauzwa ikiwa katika ubora na muonekano mzuri, inakuja baada ya filamu kutoka nje, kuuzwa kwa bei ya chini kabisa na kuleta ushindani pamoja na kuwa sinema hizo hazilipiwi kodi tofauti sana, nakuzifanya zinunulike sana kuliko filamu za ndani kutokana na bei yake kuwa ndogo.
Kampuni ya Steps Entertainment ilifanya utafiti ili kujua ni jinsi gani filamu zinatoka mbali na bado zinawafikia walaji kwa bei ya chini ni baada ya utafiti huo ndipo Kampuni ya Steps Entertainment iliamua kujibana na kufanikiwa kuingiza na kufunga mtambo mkubwa wakisasa kuzalisha cd/dvd, kuzirekodi na kuziprinti hapa hapa nchini.
Tofauti na siku za nyuma ambapo ilikuwa inaagiza cd/dvd kutoka nje ya nchi na kuja kuzirekodi tu, sambamba na mtambo huo pia kampuni hii imeamua kubuni kifungashio kipya yaani kasha za cd/dvd, ambayo ni za bei nafuu, zinamuonekano mzuri zaidi, ni rahisi kuhifadhi, nirahisi kusafiriha na nirafiki wa mazingira.
Mtambo mkubwa na wakisasa pamoja na kifungashio kipya vimepunguza sana gharama za kuzalishia nakala za dvd na cd na hivyo Steps imeona ni vyema kuonyesha moyo wa uzalendo kwa wateja wake kwa kuwapunguzia bei ya kununua filamu kwa kuwauzia kwa nusu ya bei ya awali.
Kampuni ya Steps Entertainment inaamini kuwa kitendo cha kupunguza bei za filamu zake, kitawanyima Maharamia ulafi na wizi wa wazi kabisa, kama kampuni inakaribisha wadau wote wanaosambaza filamu kwa kuja kwetu kuzalishiwa filamu zao kwa bei rahisi sana ili huyu Gaidi mkubwa anayenyonya kazi zetu aache.
- Kinaonyesha moyo wa uzalendo lakini pia kitapandisha mauzo ya filamu za kitanzania ambapo kwa ujumla wake itaongeza kipato kwa wasanii na kuchangia pato la Taifa.
- Kitapunguza uharamia wa filamu kwa kuwa bei itakuwa chini hivyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua nakala halisi.
- Kitaziwezesha library zinazokodisha filamu kuacha kukodisha na badala yake kuanza kuuza moja kwa moja
Hivyo basi Kampuni ya Steps Entertainment inamaliza mwaka 2014 na kuingia mwaka 2015 kwa kubororesha bidhaa zake, zikiwa katika ubora na muonekano wa kuvutia kwenye kasha la bahasha ngumu, bidhaa hizi zitamfikia mlaji kwa bei ya 1,500/= tu bei hii kwa filmu zitakazo kuwa katika kifungashio kipya pekee filamu zitakazo kuwa katika kifungashio cha zamani yaani kasha la plastiki zitaendelea kuuzwa kwa bei ile ile na wateja watakuwa huru kuchagua aina ya kifungashio pale wanaponunua nakala za filamu za Steps
Hivyo basi Steps Entertaiment imeanzisha kampeni maalum ya “Faidika na Steps kwa bidhaa bora, Wasanii nyota, na Filamu Bora”.
Kampuni ya Steps Entertainment inawaomba wadau wote kuendelea kuzienzi filamu za kitanzania ili kukuza kipato cha wasanii na taifa kwa ujumla , kutangaza lugha ya Kiswahili na utamaduni wa kitazania.
Bei zetu zitakuwa wazi kwa maan za steps tofauti ya bei iliyoandikwa kwenye kasha ya kuonekana zikiwazimeandikwa katika kasha na mwananchi asikulaghai mtu wa Library eti usinunue hadi hakukodishe sema No.
Mwisho, Tunaiomba Serikali Chini ya Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wawasaidie wadau wa filamu kupambana na uharamia wa filamu ambao kwa sasa umevuka mipaka wezi wanafanikiwa wasanii wanabaki Maskini.
MUNGU IBARIKI TANZANIA Mungu bariki Afrika
Carlos Johns Silondwa
Mtendaji Mkuu.
Tuesday, December 9, 2014
FAINAL YA MASHINDANO YA WAZI YA TAIFA YA NGUMI YALIVYO MALIZIKA MWISHONI MWA WIKI UWANJA WA NDANI WA TAIFA
Mabondia latifa Halidi kushoto wa Kigoma na Vumilia Kalinga wa JKT wakioneshana umwanmba wa kutupiana makonde wakati wa mashindano ya taifa ya wazi yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita
Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini 'BFT' Lukelo Willilo akimvisha medali ya dhaabu bondia Robert Kyaruzi baada ya kushinda katika fainal ya mashindano ya taifa ya wazi iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita
Mabondia Siwatu Elieta kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Zulfa Macho wakati wa fainali za mchezo wa masumbwi Macho alishinda kwa point mpambano huo
Mabondia latifa Halidi kushoto wa Kigoma na Vumilia Kalinga wa JKT wakioneshana umwanmba wa kutupiana makonde wakati wa mashindano ya taifa ya wazi yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita
Mfanya biashara na mdau na promota maarufu nchini Zahoro Maganga akisalimiana na bondia wakati wa fainali ya mashindano ya taifa.
Picha zote na SUPER D BOXING NEWS
Monday, December 8, 2014
ILIVYOKUWA WAKATI IDRIS ANACHUKUA USHINDI WA BBA- HOT SHOT 2014
MSHIRIKI KUTOKA TANZANIA, IDRIS AIBUKA NA USHINDI KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA - HOT SHOT

Idriss
RAIS KIKWETE APANGUA TENA WAKUU WA MIKOA
Rais Jakaya Kikwete
Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amempandisha cheo Mkuu wa Wilaya ya
Karatu, Daudi Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuwahamisha vituo
vya kazi wakuu wengine sita wa mikoa kuanzia jana.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
ilisema Ntibenda ataapishwa leo, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.
Wakuu wa mikoa waliohamishwa ni Elaston Mbwilo anayetoka Manyara kwenda
Simiyu kuchukua nafasi ya Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera anahamia Manyara kutoka Morogoro
na nafasi yake inachukuliwa Dk Rajabu Rutengwe kutoka Tanga alikokaa kwa
mwezi mmoja akitokea Katavi.
Magalula Magalula amehamishiwa Tanga kutoka Lindi ambako naye alikaa kwa
mwezi mmoja akitokea Geita na nafasi yake inazibwa na Mwantumu Mahiza
kutoka Pwani.
Mhandisi Evarist Ndiliko amehamishiwa Pwani kutoka Arusha alikohamia
hivi karibuni kutoka Mwanza.
Katika taarifa yake, Balozi Sefue alisema wakuu wengine wa mikoa
wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.
Uhamisho huo umekuja ikiwa ni mwezi mmoja kamili tangu Rais Kikwete
alipofanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa mikoa na kuwahamisha sita huku
wengine watatu wakipangiwa kazi nyingine.
Wakuu wa mikoa wanne wapya ni Dk Ibrahim Msengi (Katavi), Amina Masenza
(Iringa), Halima Dendego (Mtwara) na John Mongella (Kagera).
Kabla ya kuteuliwa, Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mwanza;
Dk Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kilimanjaro na Mongela
alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Walioachwa kwa ajili ya kazi nyingine ni Dk Christine Ishengoma
(Iringa), Kanali Fabian Massawe (Kagera) na Kanali Joseph Simbakalia
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, ambaye tayari ameteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo
ya Nje (EPZA).
Sorce- gazeti la Mwananch 08/12/2014
Subscribe to:
Posts (Atom)









































