b..

B1

Wynem

animation

Monday, September 13, 2010

DIRA YA MTANZANIA YAMTOLEA UVIVU SHEIKH YAHYA NA IKULU.

Hili ndio gazeti la Dira ya mtanzania linavyoonekana kwa mbele.
Na huu ndio ukurasa wa pili unavyioonekana.

Na huu ndio mpango mzima kuhusu sakata lenyewe. Lipo ukurasa wa 8 na 9 a.k.a center.

CHADEMA YAFUNIKA BUNDA.

Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ),Dk.Willibrod Slaa,akiwahutubia maelfu ya Wananchi wa mji wa Bunda,Kwenye uwanja wa Sabasaba katika mfululizo wa kampeni zake jana

Grand Malt yakusanya maelfu Coco beach

Mfalme wa Rymes afande Sele akiwa jukwaani huku akipagawisha mashabiki waliofurika katika fukwe ya coco beach jijini dar, jana j'pili katika bonanza la Grand Malt.
  
Washereheshaji wa shughuli a.k.a Wasema chochote au MC's wa bonanza la Grand Malt wakienda sambamba na mmoja wa vijana waliopanda jukwaani kuonyesha vipavi vyao.
  
Hahahahahahah! Pia mambo ya taarabu yalionyeshwa na vijana wa kike katika bonanza la Grand Malt lililofanyika jana katika fukwe ya coco beach jijini dar.
 
 Hapa Temba, pale Chege kiujumla ni TMK Family wakifanya vitu vyao katika bonanza la Grand Malt lililofanyika jana katika fukwe ya cocobeach jijini dar.
  
Na hili ndio nyomi lililokuwepo pande zile kuliokokuwa kukifanyika bonanza la Grand Malt jana pale katika fukwe ya coco beach

Thursday, September 9, 2010

TUMUUNGE MKONO SUGU KATIKA HARAKATI ZA KULIKOMBOA JOMBO LA MBEYA MJINI.

Tuungane kiukeli katika kufanikisha huu ushindi kama kweli wewe unahitaji maendeleo basi ni lazima utatakiwa kuchagua wanaharakati kama huyu (JOSEPH MBILINYI)
TUMUUNGE MKONO MWANAHARAKATI HUYU KATIKA KULIKOMBOA JIMBO LA MBEYA MJINI.

EID MUBARAK

 
Hii ni picha inayoonyesha eneo la alqa-aba ambapo ni sehemu takatifu waislamu wanayoielekea wakati wa kuswali
Huyu ndio mtoto wa kitaa akiwa katika vazi la kanzu bana.

Mtoto wa kitaa kama kawa anawatakia watazamaji / watembeleaji wote wa blog hii Kheri ya sikukuu ya eid el-fitri.

HAWA NDIO WASHIRIKI WOTE WA VODACOM MISS TANZANIA 2010.

Wednesday, September 8, 2010

ALLIANCE FRANCEE WATANGAZA MICHONGO KWA WASANII

Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Utamaduni cha Ufaransa, Didier Martin (Katikati) akiwasilisha mada yake iliyohusu Mchango wa Asasi kama yake Kwenye kukuza Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania.Kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego na Ruyembe Mulimba
Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego (Kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Alliance Francee, Didier Martin muda mfupi baada ya kuliahirisha Jukwaa la Sanaa hadi Jumatatu ijayo ambapo Mada kuhusu Changamoto za Sanaa ya Unenguaji Itawasilishwa.
  
Mkongwe wa Muziki wa Dansi, Hussein Jumbe yeye alitaka aelezwe ni kwa Jinsi gani ataweza kushiriki Tamasha la Sauti za Busara ambalo limekuwa likidhaminiwa pia na kituo hicho.
Msanii wa Kizazi kipya Symon John aka Gheto King akichangia hoja kwenye Jukwaa la Sanaa
 Sehemu ya wadau wa Jukwaa la Sanaa wakifuatilia kwa makini wasilisho la Mkurugenzi wa Alliance Francee, Didier Martin


========= ======== =======


ALLIANCE FRANCEE WATANGAZA MICHONGO KWA WASANII
Kituo cha Kimataifa cha Utamaduni cha Ufaransa (Alliance Francee) kimewataka wasanii wa Bongo kutumia programu yake ya Barazani katika kutangaza kazi zao na kuzifanya zitambulike na kupata soko kimataifa.

Barazani ni programu ya ‘pafomansi’ za kisanaa ambayo imekuwa ikiwahusisha wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na imekuwa ikifanyika kwa mwezi mara moja kwenye kituo hicho cha utamaduni.Mwezi huu itafanyika Tarehe 15.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwa kuandaliwa na BASATA likishirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz),Mkurugenzi wa Kituo hicho BW.Didier Martin alisema kwamba, wasanii hawana budi kulitumia jukwaa hilo katika kuuza na kutambulisha kazi zao kwani limekuwa likihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani.
Alisema kwamba, ushiriki wa wasanii kwenye jukwaa hilo uko wazi kinachotakiwa ni wasanii wenyewe kuchangamkia fursa hiyo kwa kufika kwenye kituo hicho na kujiandikisha.

Aidha, alisema kwamba, kwa sasa kituo hicho kinatoa mafunzo ya lugha ya Kifaransa kwa watu mbalimbali na kuongeza kwamba, gharama za malipo zimepunguzwa kwa wasanii hadi kwa zaidi ya asilimia hamsini hivyo ni fursa pekee kwa wasanii kujifuna lugha hiyo ya kigeni.

Kuhusu nyimbo za wasanii wa muziki kusikika redioni,alisema kwamba, Ufaransa imefungua kituo cha redio ambacho kitarusha matangazo kwa lugha ya Kiswahili na kuongeza kwamba, mwezi ujao wanatazamia kuanzisha dawati la Kiswahili.Bila shaka wasanii wanaobanwa kwenye ‘ea taim’ watumie fursa hiyo.

Masuala ya msingi yaliyojadiliwa kwenye jukwa la sanaa Jumatatu hii na wadau wengi ni pamoja na haja ya kituo cha Alliance Francee kupenya hadi vijijini, kusaidia kuhamasisha wawekezaji wa Kifaransa kujenga studio za kurekodia nchini, kusaidia usambazaji wa kazi za wasanii,kutoa msaada wa kifedha kwa wasanii nchin, kuzitangaza kazi za wasanii wa ndani nje ya miapaka nk.

Akijibu masuala hayo, Mkurugenzi Martin alisema kwamba, kwa sasa kituo chake kinatoa msaada wa fedha kwa wasanii wanaofanya sanaa zenye uasili wa Tanzania na kusisitiza kwamba, wasanii wa Tanzania lazima waachane na dhana ya kunakiri kazi kutoka nje bali wajikite kwenye kutengeneza kazi za sanaa za asili.

Aliongeza kwamba, tatizo la masoko ya kazi za Sanaa ni kubwa lakini akasisitiza kwamba, wasanii wanapaswa kujikita kwenye ubunifu wa kazi zilizo bora na zenye kubeba asili ya Tanzania ili kuzifanya kuwa tofauti na zile zinazotolewa sehemu zingine duniani.


Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonce Materego alisema kwamba, Baraza lake litaendelea na utaratibu wa kuwapa wasanii fursa mbalimbali za kukutana na wadau wa sanaa wa ndani na nje hata hivyo naye akakumbusha kitu ambacho ambacho muda wote amekuwa akikisisitiza cha wasanii wetu kubuni kazi zenye asili ya kwetu.

Alisema kwamba, kunakiri kila kitu kutoka nje maana yake ni kudumaza sanaa yetu na hivyo kuwafanya wasanii kushindwa kushindana kwenye masoko kutokana na kutengezeza kazi zinazopatikana kwingineko duniani.
Picha/ Habari na Afisa Habari wa BASATA, Alistide Kwizela

Monday, September 6, 2010

TUWAEPUEKE SANA VIONGOZI WA DIZAINI HII.

Kama kiongozi anaweza kutumia fedha nyingi kuliko zile atakazoenda kulipwa kama posho kule mjengonui (Bungeni) wewe unadhani ataweza kukuletea maendeleo kweli!? hapa ni lazima ataanza kurudisha kwanza zile alizozitumia ndio kama itawezekana awakumbuke baadae na hapo muda utakuwa umekwisha. Kupata katuni kama hizi tembelea ww.sidymic.blogspot.com
TUMIA VIZURI KURA YAKO

HALIMA MDEE ATEMA CHECHE JIMBO LA KAWE.

Kamama kawa kama dawa mtoto wa kitaa jumapili huwa nakuwa nimetulia tu kitaani kwangu. nikiwa katika misele ya hapa na pale kitaani kwangu si ndio nikasikia sauti kama za mziki hivi zikisikika si ndio nikasema ngoja nijisogeze nicheki kuna kitu gani kinaendelea kitaani kwangu kwa maana siku zote za wiki mtoto wa kitaa nipo na pilika za ujenzi wa hili taifa letu. Kusogea si ndio nikamgumia mdada makini kabisa ambae nkitaaluma ni mwanasheria na kutokana na uwezo wake wa kaza aliweza kulitingisha bunge lililopita akiwa katika vit maalum. Na sasa yupo kikazi zaidi akiwa ndio mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la kawe kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHDEMA). Halima Mdee kwa sasa anaendelea na mikutano yake ya kampeni katika jimbo lake ila jana alikuwa kitaani kwetu katika kitongoji cha kawe mzimuni akizungumza na wananchi wa pande zile ambao ndio wapiga kura wake!
Mdee aliongea mambo mengi sana lakini cha misngi alikua anomba tu kura! kauli mbiu yake ni
VIJANA WA KAWE TUAMKE, TUSIDANGANYIKE!

Hapa Halima Mdee akiwa anamwaga sera zake jukwaani.
Hawa ndio baadhi ya wadau waliofika kwenye mkutano huo.
  
Ilifika hatua ya kumtambulisha mama yake mzazi kwa wapiga kura wakena Halima Mdee alifanya kama anavyoonekana
Huyu ndio mama mzazi wa Halima Mdee
Baada ya kuteremka jukwaani alikutana na mwandishi wa habari na aliulizwa maswali mawili matatu na aliyajibui kikamilifu!

Saturday, September 4, 2010

MAMBO YA KUMSAKA MALKIA WA REDDS HAYA.

Baadhi ya Warembo watakaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010,ambao pia usiku wa kuamkia leo walikua katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Balozi wa Redd's 2o1o katika fukwe za Mbalamwezi Beach Mikocheni jijini Dar,Wageni waalikwa mbalimbali walihudhulia tukio hilo.mshidi atatangazwa siku ya Mashindano ya Miss Tanzania tarehe 11/09/2010 na atakabidhiwa zawadi zake siku hiyo.

Wednesday, September 1, 2010

Risechi ya mtoto wa kitaa pande za tandale kwa tumbo na maeneo ya karibu.

Hapa mwana wa kitaa nilifika katika ofisi za serikali ya mtaa wa tandale kwa tumbo na nilipokelewa vizuri na uongozi ambao walitupa mwenyeji wa kutuzungusha kila kona na kuweza kuongea na wananchi tofautitofauti.
Hawa ndio vingozi wenyewe wa mtaa.
Hapa kazi ilianza na hapa nilikuwa naongea nakina mama. 
Tukapita pita mitaani bana na hapa ni makazi ya watu. Huyu mshkaji anaitwa Nassoro Mzee ndio alikuwa mwenyeji wetu.
kama kawaida mtotowa kitaa ni mpenzi wa watoto na pia napendwa na watoo hivyo watoto hawakua nyuma katika kunipa kampani
pia nilipita mahali ambapo unaweza kuona mazingira ya upande mwingine huku pakiwa pametenganishwa na bonde kubwa ambalo pia ni mkondo wa maji.

nikaendelea kukata mitaa.
hiki ndio choo kinachotumika na moja kati ya kaya (nymuba) pande za tandale
Mazingira ndio kama yanavyoonekana
Mimi niakchoka bana ikabidi mwanangu tulio ongozana nae aendelee na mchakato mzima. Alex Peter Nyaganilwa (father P) akiongea na bibi anaeishi tandale.
Tukafika kwenye banda la kuonesha video Alex akazungumza nao. 
Kama kawa michezo ya watoto wa uswazi ni kupika matope. 
Tulifika mahali ikabidi tupumzike kwa maana uchovu wa mzunguko ukiuchanganya na mfungo yaani ni balaaa!