Mkurugenzi wa Kampuni ya
Haakneel Production Emmanuel Mahendeka ambayo ni waandaaji wa Siku ya Msanii akimwongoza
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo
Profesa Elisante Ole Gabriel kutia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili
kuzindua matukio ya Siku ya Msanii (SYM, 2016) kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa
Alliance Francaise mwishoni mwa wiki.
Katibu Mtendaji wa Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ndilo mbunifu na mmiliki wa maadhimisho ya Siku
ya Msanii nchini Godfrey Mngereza (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi (Katikati) na
Mkurugenzi wa Kampuni mwendeshaji wa Siku ya Msanii ya Haakneel Production
Emmanuel Mahendeka mwishoni mwa wiki kwenye uzinduzi wa Matukio ya Siku ya
Msanii kwa mwaka 2016 katika Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam.
Msanii maarufu wa kughani
mashairi nchini Mrisho Mpoto akisaini kitabu cha wageni kabla ya kushuhudia
hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016. Uzinduzi huo
ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise ulioko jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji
Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi. Vivian Shalua (Kushoto)
akifuatilia kwa makini moja ya matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye hafla ya
uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance
Francoise mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Msanii wa Sanaa za Ufundi Gozbetha
Rwezaula.
Marais wa Mashirikisho manne ya
Sanaa nchini kutoka kushoto Symon Mwakifamba (Filamu), Adrian Nyamangale
(Ufundi), William Chitanda maarufu kama MC Chitanda (Sanaa za Maonesho) na Addo
November (Muziki) wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali ya uzinduzi wa
matukio ya Siku ya Msanii mwaka kwa mwaka 2016
Kikundi cha Sanaa cha Safari
kikitoa burudani kwenye hafla ya Uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa
mwaka 2016 iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise
jijini Dar es Salaam
Msanii maarufu wa Sanaa za
Uigizaji na Filamu Ahmed Olutu maarufu kama Mzee Chiro akitabasamu na Msanii
mwenzie Thecra Mjata wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii
kwa mwaka 2016 uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio ya
hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016