b..

B1

Wynem

animation

Friday, January 31, 2014

TAARIFA KUTOKA IKULU JUU YA UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA.

 
Rais Jakaya Kikwete.

*****
Hatimaye, wajumbe 201 kutoka katika majina ya wawakilishi 2,722 wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na taasisi za kidini yaliyopelekwa Ikulu kwa ajili ya uteuzi wa Rais wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamepatikana.

Wajumbe hao wamepatikana baada ya kazi ya kuchambua majina hayo kufikia tamati.


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Salvatory Rweyemamu, aliliambia NIPASHE jana kuwa mchakato wa kuchambua majina hayo umefikia mwisho na sasa yatatangazwa wakati wowote kuanzia sasa.


“Process (mchakato) imefikia mwisho, wakati wowote (majina ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioteuliwa na Rais) yatatangazwa,” alisema Rweyemamu.

Jumatano wiki iliyopita, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, kuwa Rais Jakaya Kikwete, anakusudia kukamilisha uteuzi wa wajumbe hao baada ya kushauriana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), mwanzoni mwa wiki ijayo.

Alisema baada ya uteuzi huo, majina hayo yatachapishwa kwenye Gazeti la Serikali kama kifungu cha 22 (3) cha Sheria iliyotajwa inavyomtaka kufanya.

Kwa mujibu wa aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, idadi ya wajumbe kutoka Zanzibar haitapungua moja ya tatu ya wajumbe wote.

Wajumbe 20 watatoka kwenye mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na nusu yao watakuwa wanawake na moja ya tatu kutoka Zanzibar.

Wengine ni wajumbe 20 kutoka taasisi zote za dini, wajumbe 42 kutoka vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

Vyama vya siasa 21 nchini, hivyo kila chama kitapeleka wajumbe wawili na mgawanyo utakuwa huo huo.

Wajumbe wengine na idadi yao kwenye mabano ni taasisi za elimu ya juu (20), makundi ya watu wenye ulemavu (20), vyama vya wafanyakazi (19), vyama vinavyowakilisha wafugaji (10), vyama vinavyowakilisha wavuvi (10) na vyama vya wakulima (20).

Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013, Bunge Maalumu la Katiba litakuwa na jumla ya wajumbe 635.

Kati ya wajumbe hao, wanaotoka katika mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na taasisi za kidini ni 201, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni 358 na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ni 76.

Kati ya wajumbe 201 kutoka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na taasisi za kidini, nusu watakuwa wanawake na nusu nyingine watakuwa wanaume.
Wizara hiyo ilieleza kwamba wanawake watakuwa 101 na wanaume 100.

Bunge Maalumu la Katiba, ambalo litafanyika kwa siku zisizozidi 70, linatarajiwa kuanza rasmi katikati ya Februari, mwaka huu, kwa ajili ya kujadili na kuipitisha rasimu ya pili ya Katiba iliyopendekezwa.

Rasimu hiyo itawasilishwa katika Bunge hilo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Tayari Tume hiyo ilikwisha kuikabidhi rasimu hiyo kwa Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, Desemba 30, mwaka jana.
CHANZO: NIPASHE

Thursday, January 30, 2014

TOP 5 YA WABUNGE WAREMBO WENYE MVUTO BUNGE LA TANZANIA

 
1. CATHERINE MAGIGE (CCM)
 
2. VICK KAMATA (CCM)
 
2. VICK KAMATA (CCM)
 
4. MARRY MWANJELWA (CCM)
 
5. ESTER MATIKO (CHADEMA)

NI WHITE VS BLACK PARTY @ ISUMBA LOUNGE, JUMAMOSI HII

THIS SATURDAY @ISUMBA LOUNGE(JOLLIES CLUB) W.V.B
Dress in white v/s black with the LEGENDS
- karibu sana.

Wednesday, January 29, 2014

BREAKING NEWS!!!! JENGO LA GOROFA SABA (7) LAWAKA MOTO MAENEO YA KAMATA, KARIAKOO, JIJINI DAR ES SALAAM.

#HABARI Jengo jipya la ghorofa 7 (maarufu kama Jengo la Madawa) lililopo eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam, linawaka moto mkubwa katika sehemu ya kuhifadhia vitu iliyopo kwenye jengo hilo.
Jengo jipya la ghorofa 7 (maarufu kama Jengo la Madawa) lililopo eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam, linawaka moto mkubwa katika sehemu ya kuhifadhia vitu iliyopo kwenye jengo hilo.

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM KUFANYIKA KITAIFA MKOANI MBEYA

Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa Habari.

Na Mwandishi Wetu
Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangu kuanzishwa kwake Februari 5 mwaka 1977, Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa Watanzania, kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi. Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.

Kilele cha sherehe hizi kitakua tarehe 2 Februari, jambo ambalo Nape amelifafanua “Ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”

Sherehe hizi zitahitimishwa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti  wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama, Rais Jakaya Mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya.
Baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.


WanaCC waliopo mkoani Mbeya wameombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe 2.
Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali mbali nchini kote, ikiwa pamoja na shughuli za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti, kushiriki shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati, usafi pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.

PATA CHANZO CHA MSANII WA BONGO MOVIE KUJINYONGA GESTI

 
 Marehemu Victor Peter enzi za uhai wake.

Na Mwandishi Wetu
MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie amefariki dunia usiku wa juzi kuamkia jan 28/01/2014 kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo,tulipofatilia tukio hilo ilifanikiwa kuongea na mmoja kati ya wasanii walioshirikishwa na marehemu katika filamu yake ya
mwisho kabla ya kujinyonga huku filamu yake ya kwanza ikiwa bado haijatoka na kuingia sokoni yenye jina la CHOZI.
Msanii huyo aliyetambulika kwa jina la usanii Koba aliiambia kwamba siku moja kabla ya tukio Victor alifanya nao Shuting ya filamu iliotambulika kwa jina OUR FAMILY ambayo ilikuwa ndio filamu ya marehemu Vicktor ya pili tangu ajikite katika tasnia ya filamu Bongo Movie,

MSEMAJI
Cha kushangaza ni kwamba filamu hiyo muhusika mkuu alikuwa ni marehemu Vicktor na katika filamu hiyo alicheza kwamba kuna msiba baba yake kafa na yeye mwenyewe mwisho wa filamu Picha yake hiyo mnayoiona hapo juu ilipigwa Ex na muhusika aliyecheza kama mdogo wake, Matokeo yake alivyomaliza kushut aliondoka na wasanii kadhaa wakaelekea katika ATM iliokwepo maeneo ya mjini kutoa hela ili awalipe wasanii walihusika katika kazi yake,

KABLA YA TUKIO
Kwa bahati mbaya ATM machine ikagomagoma kwa tatizo kidogo la kimtandao katika kusubiria mtandao ukae sawa marehemu Vicktor alibadilika na kuonekana kama amechanganyikiwa na kuonekana hayuko sawa, Basi kwa bahati nzuri baada ya mda mchache ATM ilikaa vizuri na yeye mwenyewe ile hali ikatulia akatoa hela wakaelekea Hospitali ya Ngamiani huko mkoani Tanga, Kufika Ngamiani daktari akatoa tamko kwamba apelekwe Hospitali kuu Bombo. 

UCHUNGUZI
Kufika Bombo akapimwa kila kitu na kukutwa mzima hana tatizo lolote lile ikabidi warudi Gest walikofikia huko maeneo ya Kisosora, Marehemu akawalipa wasanii wote na kuwauliza kuwa kuna mtu anaemdai? Wakamjibu hakuna. Kila msanii akaingia chumbani kwake na kuendelea na zake, Kwa wakati ule marehemu aliingia chumbani kwake na kwakuwa ni Self Contain si rahisi kumuona mtu akitoka nje hovyo hovyo.

TUKIO
Asubuhi yakuamkia jumanne 28/01/2014 Wasanii wenzake walimgongea mlango wakaona kimya wakapatwa na wasiwasi ikabidi wamuite mwenye Gest na kusimulia hali halisi mwenye Gest akachukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mwenye kiti wa Serikali za mitaa mwenye kiti akatoa taarifa Polisi, Gari ya Polisi ikatia timu katika eneo la tukio na kuvunja mlango wakakuta mwili wa marehemu Victor ukiwa umening'inia kama unavyoonekana hapo pichani alitumia mkanda wake mwenyewe wa kiunoni kujinyongea. Vicktor kajinyonga na kuiaga dunia.
 
MWILI WA MAREHEMU
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali kuu ya mkoa wa Tanga Bombo. Marehemu ni mkazi wa mwanza na ameacha mke na mtoto mmoja, Mpaka sasa baadhi ya ndugu wa marehemu tayari wameshafika na wengine wanatarajiwa kufika kesho wa taratibu za kusafirisha mwili kwa maziko. 'Alisema Koba'
tunawapa  pole ndugu jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo, M/mungu ailaze roho ya marehemu mala pema peponi. R.I.P Vicktor.

Tuesday, January 28, 2014

MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNI USIKU HUU


MCD.JPG.jpg
MCD enzi ya uhai wake

Mpiga Tumba mahiri katika muziki wa dansi hapa nchini, Soud Mohamed, ambaye pia alifahamika sana kwa jina la MCD, amefariki Dunia usiku huu  katika hospitali ya KCMC mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro alikokuwa amepelekwa kwa matibabu. MCD ambaye alikuwa na bendi ya African Stars a.k.a Twanga Pepeta na baadae akahamia bendi ya Mashujaa Band na Kurudi tena Twanga Pepeta amepatwa na mauti hayo usiku huu, Taarifa za kifo cha MCD zimethibitishwa rasmi na Msemaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Hassani Rehani.
Tutazidi kupeana taarifa za msiba huu kwa kadri  zitakavyokuwa zikitufikia.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
AMIN.

Chanzo - MTAA KWA MTAA

MASHINDANO YA NGUMI MKOA DAR ES SALAAM YAANZA ILALA


Mwenyekiti wa Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es salaam DABA akimkabidhi risara Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu wakati wa mashindano ya wazi yaliyoanza jumatatu

Bondia Husein Pendeza  wa Klabu ya Ashanti Ilala kulia  akimtupiana makonde kiufundi na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindano ya wazi mkoa wa Dar es salaam yanayoenderea katika ukumbi wa panandi pasnandi Ilala Bungoni Ibrahimu alishinda kwa point.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu
SHILIKISHO la ngumi za ridhaa Mkoa wa Dar es salaam umezindua rasmi mashindano yake ya kwanza tanga waingie Madarakani mashindano hayo yalifunguliwa jumatatu na mgeni rasmi
Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu ambayo imekutanisha zaidi ya timu ishirini na mabondia 60 wa mkoa huu akisoma risala kwa mgeni rasmi
Mwenyekiti wa ngumi mkoa wa Dar, Akaroli Godfrey amesema mbali na mashindano hayo kuwa na changamoto mbalimbali wameamua kuyafanya kwa kuwa yapo kwenye karenda yao ata hivyo akuna zawadi zozote kwa mabondia watakaopigana hivyo kama mbunge wa jimbo la ilala tunaomba utupatie angarau medali kwa mabondia aidha vifaa tulivyo navyo avikizi kimchezo
akijibu risara hiyo mbunge huyo ame haidi kutoa zawadi pamoja na kuwa mlezi wa ngumi za ridhaa mkoa wa Dar es salaam na kuwasaidia kutafuta wadhamini mbalimbali watakaojitokeza kuinua mchezo wa masumbwi nchini ili ngumi zisonge mbele 
katika ufunguzi huo mabondia Anton Idoa alimtwanga kwa K,O ya raundi ya pili bondia Mohamed Mzeru huku John Cristian akimsambaratisha Omar Said, na shabani Alimasi akimdunda Saidi Kondo na bondia pekee kutoka timu ya shanti ya Ilala,Hussein Pendeza alipoteza kwa pointi na Ayubu Ibrahimu.

MSANII MAARUFU WA BONGO MUVI AJINYONGA LEO HUKO MKOANI TANGA

MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie afariki dunia kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR  ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.
Hapo pichani ni mwili wa marehemu ulivyokuwa ukipakiwa katika gari kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo, Chanzo cha habari kiliieleza website ya Masai Nyotambofu kuwa msanii huyo alikuwa katika harakati zake za kushut filamu yake mpya ambayo alicheza kama muhusika mkuu katika filamu hiyo.
Kilichowashangaza wenzake ni kwamba filamu iliisha jana Jumatatu 27/01/2014 na story ilimalizikia Vicktor kufa kwakujinyonga matokeo yake leo alfajiri Victor akakutwa amejinyonga kweli na kuiaga dunia, Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijatambulika.
Ndugu msomaji taarifa kamili na picha za tukio zima la kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka Hospitali na mengineyo fatilia hapa utayapata hivi punde.

Monday, January 27, 2014

"NEW AUDIO" Anapita ft Hellen-Tunaweza (Seductive Recs)

Mwanadada Anapita akishirikiana na Hellen wanakwambia "Tunaweza", ikiwa ni ngoma mpya toka Seductive Records chini ya mkono wa Mr.T Touch, kudownload/kusikiliza bofya HAPA

Thursday, January 16, 2014

ALICHOKISEMA B12 JUU YA YEYE KUSIMAMISHWA KAZI CLOUDS FM

 
Hamis Mandi aka B12 mkali wa pindi la XXL ni miongoni kati ya watangazaji wa Clouds walio subirishwa kazi ya utangazaji kutokana na madai ya chinichini ya kuwa wamekiuka sheria na taratibu za Clouds Media inavyotakiwa kuendeshwa.
Baada ya chanzo chetu kuzinasa taarifa hizo, kiliamua kumvutia wire B12 live bila chenga naye akamwagika kimtindo huu,
“Mimi bado nipo Clouds media sema tu sipo kwenye kipindi now lakini mwezi wa pili nitakuwa ndani ya kipindi ukitaka full details zungumza na uongozi wa Clouds Media hope utafahamu zaidi things follow apart” – B12

NGUMI KUPIGWA MKOA WA PWANI IJUMA


Na Mwandishi Wetu
NGUMI kupigwa mkoa wa Pwani  mchezo wa masumbwi unatarajia kufanyika siku ya ijumaa katika ukumbi wa Shimbikati  pub uliopo Kiluvya Mkoa wa pwani mpambano  mchezo wa ngumi katika mkoa wa pwani umendaliwa na kocha wa mchezo huo Jafar Ndame
akizungumzia mpambano huo ambao unasubiliwa kwa hamu na wakazi wa kiluvya pamoja na vitongoji vyake litawakutanisha mabondia Azizi Abdallah atakaepambana na Sadam Manjapa uku Julius Kisarawe akivaana na Haji Gamba, na Tasha Mjuaji akimkabiri roja mjeshi na mapambano mengine mengi ya utanguliza pamoja na burudani nyingine nyingi
Mipambano hiyo ya masumbwi yatakuwa chini ya chama cha ngumi za kulipwa PST na Rais wake Emanuel Mlundwa ambao ndio wasimamizi wakuu wa mchezo huo siku hiyo
mbali na kuwepo kwa mchezo huo wa masubwi pia kutakuwa na huzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi wakiwemo mabondia wak
ali kama vile Floyd Maywether,Manny Paquaio,Oscar Dela Hoya,Mohamed Ali,mike Tyson, pamoja na mabondia mbalimbali pia kutakuwa na vifaa vya mchezo wa masumbwi kama vile glove,gumshiti,clip bandeji na vifaa mbalimbali vitakavyokuwa vikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masum,bwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huo ili wapenzi wajue sheria na taratibu za mchezo wa masumbwi

Wednesday, January 15, 2014

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KONGAMANO LA WASANII IJUMAA (january 17)

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher' 
(kushoto)
 
 Mwandishi Wetu.
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa kongamano la umoja na mshikamano linalofanyika Januari 17 (Ijumaa) kwenye viwanja vya hoteli ya Lamada ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema madhumuni ya kongamano hilo ni kuhamasisha umoja kati ya wasanii ili kujenga uwezo na nguvu ya kumaliza matatizo yao ya kiuchumi.
Alisema wasanii, waandishi, wa habari na Vijana wanashindwa kumaliza matatizo yao ya kiuchumi bila kuombaomba au kusubiri misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali.
"Wasanii inatubidi tujifunze kujitegemea na tuache kusubiri wafadhili au serikali ituchangie hata kwa matibabu na katika mazishi yetu" alisema Taalib.
Katika kongamano hilo Shiwata itazingua mpango maalum ambao utawezesha wasanii kupata misaada ya fedha za kutengeneza filamu,kurekodi muziki,kuwezesha timu na vikundi mbalimbali kununua vifaa vya ichezona kuwapatia nauli ya usafiri ndani na nje ya nchi kwa shughuli za michezo na sanaa.
Katika Mpango huo Shiwata pia itatoa fedha kwa mrithi wa msaniii kamaatakufa, akiugua au kulazwa kwa siku tatu katika hospitali zinazotambuliwa na Serikali.
Alisema Shiwata pia itatoia misada kwa wasanii wanaotaka kuoa au kuolewa ambako kila mwanachama atachangia sh. 1,000 kwa ajili ya kugharamikia mazishi ya msanii kununua sanduku n usafiri.
Alisema Shiwata itakusanya zaidi ya sh. Mil.7 kutoka kwa wanachama 7,000 na wasanii watajiunga kwa sh. 20,000 ambazo zinaweza kulipwa kwa awamu tatu kutokana na uwezo wa msanii.
Sjiwata ina ekari 300 za makazi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga ambapo hivi sasa kuna nyumba 40 zilizojengwa kwa nguvu ya wasanii wenyewe na ekari 500 za kilimo.

Sunday, January 12, 2014

"NEW AUDIO" Stereo ft Ben Pol - Usione Hatari

 
Ngoma inakwenda kwa jina "Usione Hatari ya HipHop Mc maarufu kama Stereo akimshirikisha BenPol katika chorus, kazi toka studio za Noizmekah Studios chini ya Producer Defxtro,kusikiliza/kudownload click HAPA

Thursday, January 9, 2014

"NEW AUDIO' Kajoli Masai & Hard B - Ndani Ya Club

Hard B pamoja na Kajoli Masai na ngoma mpya "Ndani ya club" ambayo ni category ya dancehall,kazi toka studio za Noizmekah Arusha,click HAPA kudownload/kusikiliza

Diamond Feat Davido - Number One Remix (Official Video)


Wednesday, January 8, 2014

MWENYEKITI WA CHADEMA WILYA TEMEKE APIGWA NA KUTUPWA USIKU WA KUAMKIA LEO

ununio3ununio4ununio6ununio1ununio1DSC_0027
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam. Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake. ‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja.. tulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’ Unaweza kusikiliza maelezo yake mengine akihojiwa kwa kubonyeza play hapa chini..

MAASKOFU WAMTEMBELEA RAIS MTAAFU, ALI HASSAN MWINYI NYMBANI KWAKE, ZANZIBAR

DCIM100MEDIA 
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa binti wa Mratibu wa Dua maalum ya kuiombea Zanzibar, Clare Allen Mbaga walipomtembelea na kumuombea nyumbani kwake Maisara ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
DCIM100MEDIA
Mratibu wa Dua Maalum ya kuiyombea Zanzibar kwa ajili ya mwaka mpya wa  2014  Allen Mbaga akizungumza na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi walipomtembelea na kumuombea nyumbani kwake Maisara ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DCIM100MEDIA
Picha ya pamoja ya Kamati maalum ya kuiyombea Zanzibar kwa ajili ya mwaka mpya 2014 na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi ilipomtembelea nyumbani kwake Maisara ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mpinduzi ya Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).

Tuesday, January 7, 2014

"NEW AUDIO" AkiliMingi ft Ordinally JamboSquad-Nafurahi (NOIZ

Msanii AkiliMingi anakuja na ngoma "NAFURAHI" akiwa amemshirikisha mwana Jambo Squad Jogoo Kichaa aka Dunia,au maarufu zaidi kama Ordinally Odii na mkono huu wa dancehall ni special kwa fans wote wa AkiliMingi na Ordinally JamboSquad umepikwa studio za Noizmekah Arusha chini ya Defxtro, bofya HAPA Kudownload/sikiliza

CHADEMA HALI BADO NI TETE

 
Mfuasi wa Chadema akiwa chini baada ya ‘kukatwa mtama’ na mfuasi mwingine wa chama hicho baada ya kutokea vurugu baina ya wafuasi wanaounga mkono uongozi na wale wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe jana baada ya kuahirishwa kwa hukumu ya kesi ya mbunge huyo katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam jana.
Picha na Silvan Kiwale source; Mwananchi 07012014

Monday, January 6, 2014

SOPRANO MUSIQ AACHIA VIDEO TURN YOUR LiGHts DoWn Low "OFFICIAL VIDEO"


BIGGIE BOSS AACHIA MIX TAPE YAKE YA SHILINGI NGAPI

Msanii BIGGIE BOSS akitambulisha Mix Tape yake pale New Msasani Club kwenye Kilinge Cha Hip Hop Juzi Jumamosi

NB:
Msanii - Biggie boss
Kanda Mseto - Shilingi ngapi
Wasanii walishirikishwa ni pamoja na:-
Stive Nyerere Cpwa, Mchiz Mox Saigon, Kimbunga, Mirror G nako Ebby Sykes
Mix Tape hii Inapatikana Sehemu zifuatazo :-
 Machapter Prod, twitter Pub, Kim Classic, Uhuru Pick Pub, Delina Beurr de Chnge, Kilinge cha Hip Hop 

Friday, January 3, 2014

BIOGRAPHY YA MSANII SOPRANO


SopRAnO alizaliwa tar 2 May 1985 Dar Group hospital Ilala Dar es salaam Tz.Ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto wa nne watoto wawili wa kike na wawili wa kiume.Primar school alisoma Yombo Primary school na baada ya kumaliza msingi alijiunga na sekondari Jitegemee high school na baadae kujiunga na chuo cha UCC University college of computer.Amekulia mitaa ya kiwalani kaliagogo kijiwe samli Ilala dar es salaam.Alianza kujishughulisha na muziki miaka ya tisini lakini akaanza kurekodi santuri yake ya kwanza iliyoitwa HOFU iliyofanywa na producer MANECKY studio za Midman Rec mwaka 2005.Lakini hakuitoa mwaka huo kutokana na kuwa bado hakumaliza shule,Mwaka 2006 baada ya kumaliza shule aliiachia santuri hiyo pamoja na video ya wimbo huo ulifanya vizuri ingawa haikuwa sana.Lakini ukampatia show za uhapa na pale.Mwaka 2008. akaachia wimbo wake mwingine ulioitwa MSHUMAA Nao pia haukufanya vizuri sana. Mwaka 2009 alikutana na Q Chief wakawa wanafanya album ya pamoja lakini cha kushangaza ndugu yake huyo akamgeuka kwa tamaa ya fedha akamtoroka mwezake na kwenda studio nyingine kurekodi wimbo wa TUTAONANA WABAYA na Kuitoa.Lakini SOPRANO hakukata tamaa nae akaifanya kipekee na kuitoa nyimbo yake ikiwa km jibu kwa q chief ikaitwa TUSHAONANA WABAYA ambayo ilifanya vizuri na kumfanya Soprano kujulikana kila kona ya bongo.Baadae akaachia wimbo mwingine uliokwenda kwa jina la SIMU YA TOCHI Na baade kuachia wimbo mwingine NASEMA GO Ambao unafanya vizuri kuanzia radio hadi tv kwa sasa na huyo ndio Francis Xaviery Ndumbaro a.k.a SOPRANO.