b..

B1

Wynem

animation

Tuesday, July 31, 2012

VIDEO MPYA YA RAMA DEE Ft MAPACHA - KUA NA SUBIRA

POLISI YAWASHIKILIA WATU 13 WAKIWEMO VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU MKOANI MBEYA

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani , akiongea na waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda wa polisi mkoa Mbeya

Na Mwandishi Wetu
POLISI Mkoani Mbeya, inawashikilia watu 13  wakiwemo viongozi wa Chama cha walimu na walimu wenyewe kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizosababisha hasara zaidi ya shilingi milioni 100 wakati wa mgomo wa walimu ulioanza juzi.
Kitendo cha walimu hao kugoma kuingia darasani kilisababisha baadhi ya maeneo, wanafunzi  kufanya maandamano ya amani ya kudai haki ya kufundishwa  jambo ambalo linadaiwa kutumiwa vibaya na wahalifu kwani walitumia nafasi hiyo kufanya uhalifu kwa kuiba mali za watu.
Wahalifu hao walichoma ofisi za Halmashauri ya Mbozi ndani ya Mji mdogo wa Tunduma  na kuiba mali zilizokuwemo kama  kompyuta 5 za ofisi, pikipiki yenye namba STK 6264, kumbukumbu na nyaraka mbalimbali.
Wahalifu hao  walivunja milango ya ofisi zote, kuvunja vioo vya magari ya kubebea taka aina FAW  SM 8726, na kuiba betri mbili za gari hilo  na gari dogo aina ya Nissan lenye namba SM 2858 mali ya mamlaka hiyo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani , aliwataja watuhumiwa hao wanaodaiwa kuhusika na uhalifu  na kusababisha hasara ya shilingi  milioni 117, 515,000  kuwa ni Mexon Mbilinyi, Akida Kondo, Chalres Rupia, Athumani Mgala, Stela Garbert, Atiliyo Benard, Nikodemus Exavely, Mashaka Amoni na James Kabuje.
Diwani, alisema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuhusika na uhalibifu wa ofisi ya halmashauri ya mji mdogo wa tunduma ikiwa na kuiba mali yenye thamani zaidi ya milioni 100 na kwamba wote kwa pamoja wamefikishwa mahakamani leo.
Akizungumzia suala la kukamatwa kwa viongozi wa Chama cha walimu pamoja na walimu  alisema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na tuhuma za kuhamasisha wezao kugoma jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Aliwataja wahusika hao kuwa ni Mwalimu wa Patro Mangula na ni Katibu wa chama cha walimu wilaya ya Kyela ambapo inadaiwa kuwa kiongozi huyo alikuwa akishirikiana na watu wengine kupita mashuleni kuhamasisha walimu waliokuwa wanaendelea na kazi ya kufundisha wajiunge na mgomo.
Wengine ni Mwalimu Emanuel Kyejo wa shule ya msingi Mbebe Wilaya ya Ileje na mjumbe wa chama cha walimu wilaya ya Ileje, Anyakingwe Lwinga na mjumbe wa chama cha walimu ambapo wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuhamasisha walimu kugoma.
Aidha, katika uhalifu wa Tunduma, Kamanada Diwani alisema kuwa polisi Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kuokoa Mabati 168, Printa moja na mita mbili za maji, Bendera moja ya Taifa na photocopy mashine.
Pia, Kamanda Diwani alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kwa nini askari wake walitumia  Bomu  na risasi katika vurugu hizo ambapo alisema kuwa Bomu hilo lilitumiwa kulitawanyisha kundi kubwa la watu lililokuwa linazidi kuelekea kwenye ofisi za serikali pamoja na Taasisi za kibenki  na kwamba hakuna madhara yaliyojitokeza.
“Baadhi ya watu wamekuwa wakiipotosha jamii kuwa askari walitumia bomu kuwatawanya wanafunzi na ndio sababu za wananchi kuanzisha vurugu jambo hilo si kweli kwani bomu lilitumiwa baada ya kundi la wahuni lililokuwa likivamia ofisi na kuiba mali zilizomo ndani,”alisema.
Alisema,  wakati kundi hilo linafanya vurugu tayari wanafunzi walikuwa wamerejea kwenye makao yao lakini kundi hilo la wahuni ndio lilikuwa likizidi kujikusanya na kuendelea kufanya uhalifu huo huku baadhi wakiwa wanaelekea kwenye eneo la Benki.
“Baada ya walinzi wa Benki kuona kundi hilo linaikaribia benki askari walipiga risasi mbili juu ili kuwatawanya na kwamba zoezi hilo lilisaidia kuwarudisha watu hao waliokuwa na lengo la kufanya uhalifu katika benki hiyo ,”alisema
Aidha,  Diwani aliitaka jamii kuondoa mawazo potofu kwamba huenda vurugu hizo zimechangiwa na baadhi ya wanasiasa jambo ambalo si kweli kwani jeshi la polisi linaamini kuwa kundi hilo la uhalifu halina itikadi yoyote ya siasa.
“Polisi inawashikilia watu hao kwa tuhuma za uhalifu na ninaamini watu hawa ni wahalifu hivyo watafikishwa mahakani kwa makosa ya uhalifu tu na wala hakuna siasa,”alisema
Hata hivyo aliwataka walimu pamoja na viongozi wa chama cha walimu kuacha kuwahamasisha wezao kufanya mgomo kwani wao tayari walitangaza kugoma na wamegoma hivyo kupita mashuleni na kuwakuta wezao wanafundisha na kuwalazimisha kugoma ni uvunjifu wa amani hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa zidi yao.

BONDIA IBRAHIMU CLASS AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WA IDI PILI


Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee Bondia huyo ambaye yupo chini ya Makocha Habbu Kinyogoli pamoja na Rajabu Mhamila 'Super D' anategemea kuonesha ufundi wa ali ya juu katika mchezo wa masumbwi nchini.

Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee. 
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Monday, July 30, 2012

KAMERA YA MTOTO WA KITAA ILIPOMULIKA PANDE ZA STENDI YA MWENGE LEO JIONI


VODACOM YATOA TUZO ZA VADE 2012 KWA MABLOGGER 10

Mablogger wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuchukua Tuzo zao. Kutoka kushoto ni Millard Ayo, Dj Fetty, Masoud Kipanya, Miriam Kinunda, John Kitime, Mike Mushi na Vijana Fm.

NDOTO YA TANZANIA KUTWAA MEDALI OLIMPIKI YAANZA KUYEYUKA BAADA YA SELEMANI KIDUNDA KUPIGWA KWA POINT

Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kushoto) akishambuliwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012. Picha: REUTERS
Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kulia) akiendelea kuadhibiwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012. Picha: REUTERS
Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kulia) akiwa hoi baada ya kudundwa kirahisi kwa pointi 20-7 dhidi ya bondia wa Moldova, Vasilii Belous katika pambano la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012. Picha: REUTERS

Sunday, July 29, 2012

NGOMA MPYA KUTOKA KWA VATOLOCO - STEP ON DEM

Brand New Vatoloco the red track inayofahamika kama Step on Dem, akiwemo lavosti katika chorus na verse ya kati huku Fido akiwa kwa first and last verse za hiphop joint iloundwa pande za noizmekah.com.Step on dem is a street banger focusing on the struggles we goin through na ma snitch wanavo set back mipango ya harakati zetu.to all our fans and supporters out there,pamoja and peace ya'll..

KAMERA YA MTOTO WA KITAA ILIPOMULIKA KWENYE UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA UTAIFA PANDE ZA KAWE, JIJINI DAR


WAISLAMU WAKUTANISHWA NA TAASISI YA ALNNA JAH

Sheikh Mkuu wa chuo cha Alnna Jah cha Sheria za kiislam Fahamu Lubwaza kulia akiomba duwa baada ya kufutulu na waislam wenzake Dar es salaam jana futari hiyo ilikuwa ni moja ya kuitambulisha Taasisi hiyo ya kislamu kwa waislamu kwa kuiunga mkono
Baazi ya waumini wa kiislamu wakiomba Duwa baada ya kumaliza kufuturu wakati wa kuitambulisha Sheikh Mkuu wa chuo cha Alnna Jah cha Sheria za kiislam
Sheikh Mkuu wa chuo cha Alnna Jah cha Sheria za kiislam Fahamu Lubwaza kulia akifuturu pamoja na waumini wa Dini ya kiislamu Dar es salaam jana futari hiyo ilikuwa ni moja ya kuitambulisha Taasisi hiyo ya kislamu kwa waislamu kwa  na kuiunga mkono

Friday, July 27, 2012

SHIWATA YAPEWA KIBALI CHA MAPAMBANO YA NGUMI MWAKA MZIMA NA TPBC


SHIWATA yapata kibali kuchezesha ngumi nchini
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) imekubaliwa kupata kibali cha kuandaa mashindano ya ndondi za kulipwa kupitia Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia  Julai 24 mwaka huu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango vya Mabondia wa Ngumi za Kulipwa  TPBC,  Boniface Wambura alisema kibali hicho kinaruhusu SHIWATA kuandaa mapambano na la kuanzia ni kati ya bondia Alfonce Joseph (Mchumiatumbo) na David Michael Mlope (Zola D – King) litakalofanyika katika Tamasha la Watani wa jadi katika Sikukuu ya Idd El Fitri kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari Temeke.
Pambano hilo ambalo limeandaliwa na SHIWATA ili kukusanya fedha za Ujenzi wa nyumba za kisasa za gharama nafuu kwa ajili ya Wasanii, Waandishi wa Habari na Wanamichezo katika Kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.
Kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini Tanzania (TPBC) ambalo inasimamia pambano hilo la Mabondia  hawa watakaocheza katika uzani wa juu (Heavy Weight) raundi nane (8) pia kutakuwa na pambano moja la utangulizi.
Mwenyekiti wa SHIWATA Cassim Taalib alisema pamoja na pambano hilo, kutakuwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya Simba na Yanga (Veteran) katika Uwanja huo huo wa Chuo cha Bandari Temeke na mshindi wa mchezo huo atazawadiwa ng’ombe dume.
Taalib alisema kwamba kikundi cha Mchiriku cha Jagwa kitatumbuiza, Roman Mg’ande wa Msondo atapigana mieleka na Lumole Matovolwa (Big na upande wa wanawake Sophia Lubuva wa Simba atapambana na Mwajuma Jimama wa Yanga huku washangiliaji wa Mpira Pesa (Simba) watapambana  katika mpira wa miguu na Watani wao wa jadi Yanga Bomba.
Tamasha litapambwa na mechi ya Mpira wa Kikapu ya Ngongoti pamoja na mashindano ya Pikipiki ambayo yanatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa watoto na wakubwa ambao siku hiyo watakuwa wakisherekea Sikukuu ya Idd el fitri baada ya kumalizika kwa mwezi wa Ramadhani, Wasanii wa Bongo Flava nao watakuwepo.

KUMEKUCHA TAMASHA LA “CHAGGA DAY CULTURAL FESTIVAL 2012” KESHO

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Maganga (Kulia) akielezea juu ya tamasha maalum la siku ya Wachaga  lililodhaminiwa na Pepsi, litakalofanyika siku ya Jumamosi Julai 28,Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambapo pia litasindikizwa na bendi za Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na vikundi vingine vya ngoma ya asili, (Kushoto) Ni Fredrick Mtaki, Afisamahusiano wa kampuni hiyo. Picha Na Mpiga Picha wetu

Na Mwandishi Wetu
BENDI  zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
Akizungumza na waandishi wa habari  mapema leo ukumbi wa Udara habari Maelezo, ijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul  Maganga walioandaa tamasha hilo lililoadhaminiwa na kampuni ya SBC Tanzania Limited,kupitia kinywaji cha Pepsi, alisema  siku hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni  wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine  na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo,  pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema  Maganga
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa  mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema  baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe mbalimbali
Aidha, Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua mila zao  sambamba na kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa  kuwakumbusha tamaduni zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina ya  makabila mbalimbali  nchini Tanzania.
Pia anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo, watapata kujua chimbuko la kuweko kwa  tamaduni zao  yaani mashujaa wa makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii zao.
Maganga pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni pamoja naTBL kupitia bia za Safari na Kilimanjaro,  SBC Tanzania (Pepsi), Dstv,Homeshopping Centre,Canocity,Kishen Enterprises, Zizou Fashion, CXC Africa,Giraffe Hotel,BM barber shop,Mlonge Bi Makai, Chili Chili Restaurant, Auckland Safaris &Tours, Clouds Fm, and Alleys Travel &Tours, Dotnata Decorations.

Tuesday, July 24, 2012

KAMBI YA ILALA YAENDELEA KUMFUA BONDIA IBRAHIMU CLASS KWA AJILI YA MPAMBANO WA IDI PILI

Bondia Ibrahimu Class kushoto akipambana na Yohana Robart wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambnano wake na Simba Watundulu utakaofanyika siku ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee.
Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Habibu Kinyogoli katikati akiwaelekeza mabondia Yohana Robert KUSHOTO NA Ibrahimu Class jinsi ya kutupa masumbwi kwa mpizani kwa kunyoosha mkono Class anajiandaa na mpambano wake na Simba Watundulu siku ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee jijini Dar es salaam

Na Mwandishi Wetu
KAMBI ya ngumi Ilala ipo kwenye maandalizi mazito ya kumnoa bondia Ibrahimu Class 'Ibra Mawe' anaetarajia kuzipiga na Simba Watundulu katika uzito wa KG,60 litakalofanyika siku ya Idi pili katika ukuimbi wa Diamond Jublee.
 Akizungumza mmoja wa makocha wa kambi ya ilala inayongozwa na Kocha mkongwe wa  mchezo huo Habibu Kinyogoli, Rajabu Mhamila 'Super D', amesema katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wanamwandaa bondia Ibrahimu Class kwa ajili  ya mpambano huo utakaofanyika siku hiyo Super D alisema wamemuandaa bondia wao kufanya vizuri ili kuweza kumzibiti  mpinzani wake kwa kuwa wanamjua uchezaji wake awapo ulingoni hivyo wanamfundisha  mbinu mpya kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake.
Kambi hiyo ya ngumi imewataka wadau wa mchezo uho kuja kuangali mchezo mzuri wa  masumbwi utakaonyeshwa na bondia wao kutoka kambi ya ilala Ibrahimu Class anaetamba kwa jina la 'Ibra Mawe' ambaye yupo kwenye maandalizi makali chini ya makocha wake Kinyogoli na Super D kwa ajili yampambano huo na kuwataka  wapinzani wake kwa sasa wakae chonjo kwa kuwa moto umesha washwa na akuna wa  kuuzima kwa bondia huyo chipkizi na mwenye nia ya kuupaisha mchezo wa masumbwi  Kimataifa.
Mabondia hao watakuwa wakicheza katika mpambano wa utangulizi wa RAUNDI 6 uku pambano kuu ni kati ya Ramadhani Shauli wa Tanzania na Sande Kizito wa Uganda watakaopambana kugombania mkanda wa Ubingwa wa IBF se3s Afrika

TWANGA, MSONDO KUPAMBA TAMASHA LA SIKU YA WACHAGA‘CHAGA DAY 2012’

Baadhi ya wasanii wa Msondo Ngoma
Wasanii wa Twanga Pepeta

Na Mwandishi Wetu
BENDI  zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo kali na ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), siku ya jumamosi Julai 28, katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Siboka walioandaa tamasha hilo, alisema  siku hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza
Na kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni  wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine  na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo,  pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema Siboka.
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa  mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema  baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo nbalo litapambwa na sherehe mbalimbali. 

ANT EZEKIEL: NGOZI, KAZI YANGU VINANIPA DILI HAPA MJINI

MSANII na mtayarishaji wa filamu za Swahiliwood,  Aunty Ezekiel, amesema kuwa matokeo ya kuilinda ngozi yake kwa kutotumia ovyo vipodozi, yamekuwa na faida kubwa kwake.
Anasema kwa umakini huo ndo unafanya ngozi yake kuwa na mwonekano wa kuvutia hivyo kumpa nafasi kubwa ya kupata kazi katika tasnia hiyo.
"Katika maisha yangu, ngozi ina thamani kubwa. Huwa nailinda isidhurike na kemikali, vipodozi vyangu ni vya kawaida kabisa," alisema baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa ZUKU.
"Situmii kemikali kabisa na sina gharama kama wengine, najivunia mwonekano wangu wenye kuvutia pamoja na kuwa na uwezo wa kuigiza, ndiyo maana nawashika wapenzi wa filamu."
Msanii huyo pamoja na Jacob Stephen walichaguliwa kuwa mabalozi wa Zuku Swahili Movie inayotarajia kuzinduliwa mwezi ujao.
Kwa ubalozi huo, wanatarajiwa kupata mikataba ya matangazo itakayohusu bidhaa za kampuni hiyo pia kushiriki katika kampeni mbalimbali za filamu.

Monday, July 23, 2012

THIS IS CAMP MULLA BIOGRAPHY



Name: Michael Mutooni

Stage Name: Mykie Toni
Position: CEO & Hype-Man  
Age: 21
Also known as ‘Tuchi’ , the group looks up to him as their keystone social-media connector. Like a plug, he connects all Camp Mulla’s social networking with the fans. His business savvy attitude enables him to make choices and decisions that better the group and put them in a good market position.
Name: Marcus Kibuksoya
Stage Name: K’ Cous
Position: Head Producer , Song Writer
Age: 20
K Cous is known for his musical expertise; being the groups multi talented producer, he definitely takes a lot of credit for the groups current and upcoming success. The seriousness he puts into his work clearly reflects on to the impressive tracks he has produced.
Name: Karun Mungai
Stage Name: Miss Karun
Position: Lead vocalist , Song Writer
Age: 18
The vocals of Miss Karun are definitely at the level of professionals. She sings effortlessly, radiating confidence and passion for what she does. Music is definitely her forte. Her high vocal range makes her a force to reckon with and her pitch is flawless. Definitely a rising star, and one to keep your eye on.
Name: Mathew Wakhungu
Stage Name: Taio Tripper
Position: Rapper , Song Writer
Age: 18
A Co-Founder & cocky rapper is most famously known for his innovative compositions, claiming to have “the future in his hands” and being “allergic to defeat”. It’s therefore not surprising that he’s the group’s main songwriter. In the studio, he is notorious for putting one hundred and ten percent into his work, and when outside the studio, he’s busy being a top prefect and leader in high school, getting much respect and encouragement from his peers. Furthermore he is a perfectionist in all he does including his song writing and vocal passing.
Name: Benoit Kanema
Stage Name: Shappa Man
Position: Rapper , Song Writer
Age: 18
A Co-Founder & the group’s first rapper, Shappa Man is more than exceptionally talented. With a raspy unique and more than catchy voice, he steals the crown for most entertaining, where his extreme punch lines hit the jackpot. His personality is incorporated into his rhymes, eluding confidence and swag. To say he is lyrically gifted would be an understatement, he has a endowment that not many have – creativity and incredibility.
His witty banter puts him at the top of the game, daring anyone to advance.