b..

B1

Wynem

animation

Wednesday, November 30, 2011

VUGUVUGU LA ANTI VIRUS NA HOFU KUBWA YA MAFISADI WA SANAA TZ-WARAKA WA 1

Salaam nyingi kweni nyi wote wapenzi wa muziki hapa Bongo,leo kamanda wenu Mac Temba aka mwanaharakati wa Anti virus nataka kuwapa tafsiri na kuweka mambo sawa yote kuhusiana na mambo kibao yanayopindishwa na kuficha ukweli wa Vuguvugu la kudai haki sawa na uwanja huru wa kufanya sanaa hapa Bongo,kwa jina la mtaani limepewa jina la “Anti virus”
Anti virus ni mkusanyiko wa watu mbalimbali wenye taaluma mbalimbali na uwezo mbalimbali ambao tunaamini kuwa sanaa hii ya muziki inaweza kuwasaidia vijana wengi hapa bongo na pia kuisaidia nchi yetu kupata kodi ambayo itasaidia kuleta maendeleo na kuisogeza nchi yetu mbele kama wenzetu Afrika kusini,Nigeria.Kamwe huu si mgomvi na mtu mmoja wala chombo kimoja cha habari.
Kinachodaiwa hapa ni haki na usawa katika sanaa na malipo sahihi kama wanavyolipwa wakenya na wanaigeria wakija hapa kufanya maonyesho mafupi ya muda wa saaa moja na kuchota mamilioni mengi toka kwa makampuni ambayo yanapata faida toka kwa watanzania hawa ambao wasanii wao wa ndani wanaishi maisha mabovu sana na wala hawakumbukwi na makampuni haya ya bidhaa ambayo hupata mamilioni ya faida toka wa watanzania hawa.
Sanaa  na soka ni fursa pekee ya kumfanya mtoto toka katika familia masikini kuweza kuwa milionea ama kufanikiwa kujinyanyua toka katika maisha mabovu mpaka maisha bora,ni kama mpira ulivyo katika nchi ya Brazil,soma historia za wanasoka kama wakina Ronaldo de Lima na wekina Pelle soka ndilo lililowafanya waweze kujiinua na kuweza kuzisaidia familia zao kupata mafanikio na kuishi maisha bora nay a kifahari.

Tuesday, November 29, 2011

BREKING NYUUUZZZZZZ: JK ATIA SAINI MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.
Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari
ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge
kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao
kilichopita cha Bunge.
Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu
katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.
Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na
mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.
Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye
maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru
kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Novemba, 2011

RASHID MATUMLA VS MANENO OSWARD KUPIMA UKIMWI SIKU KUMI KABLA YA MPAMBANO

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.
Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.
Utasindikizwa na mabondia Venas Mponji atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa
Siku kumi kabla ya mpambano huo mabondia Rashidi Matumla na Maneno Osward wameshauliana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa ya kuongeza nguvu kama wanatumia  sheria za mchezo huo azirusu kutumia dawa za aina yoyote ya kuongeza nguvu
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.
'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,
DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

Monday, November 28, 2011

TWANGA PEPETA ILIVYODONDOSHA MAKOMBORA KUAMSHA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU LONDON

Mgeni Rasmi Mh Balozi Peter Kallaghe akifanya Toast.
Mh Balozi na Mama Balozi wakifungua mziki.
Mh Naibu waziri katika Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Aggrey Mwanri.
Twanga Pepeta katika picha ya pamoja na viongozi.

Na Freddy Macha
 African Stars Entertainment Tanzania (Aset) ambao wanajulikana kwa jina la  “Twanga Pepeta” walikuwa  kivutio cha sherehe za miaka 50 ya Uhuru London juzi Jumamosi. 
Kikosi hiki cha watumbuizaji maarufu wa Kibongo kilikaribishwa na  Urban Pulse, Jestina George wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania mjini hapa.
Watanzania wa kila rika, nasaba na taaluma walifurika toka miji ya Leeds, Bristol, Birmingham, Northampton, Milton Keynes na vitongoji mbalimbali kufurahia vigongo vya bendi hili lenye makao makuu Mango, Kinondoni Dar es Salaam. 
Ukumbi wa Club 2000 Banqueting Suite ulioko nyuma ya uwanja maarufu wa Wembley ulishuhudia tafrija hiyo wakati viongozi rasmi wa serikali walipofungua tafrija wakicheza nyimbo maarufu za Kitanzania kama ule wa mwanamuziki Salum Abdallah (“Wanawake wa Tanzania” na “Tujenge Nchi Yetu”) marehemu alizoimba mara baada ya Uhuru mwaka 1961.
Viongozi waliojumuika walikuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, Balozi wa Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, naibu wake Mheshimiwa Chabaka Kilumanga na Ofisa Habari ndani ya ubalozi, Mheshimiwa Amos Msanjila aliyehamasisha wageni kwa kunyofoa kinywaji cha “champagne” mahsusi kuzindua maadhimisho.
Akiwakaribisha wageni Balozi Kallaghe alisema sherehe za miaka 50 ni idhinisho kuwa Tanzania ni nchi ya amani inayostahili kuwa fahari yetu sote. “Waangalie Waingereza wanavyoorodhesha tarehe na mida ya majengo yao muhimu. Kutambua na kusherehekea muda kamili wa matukio ya jamii ni jambo muhimu na la kawaida,” alikumbusha kiongozi huyo na kupigiwa makofi.
Kutokana na maombi mengi ya washabiki Twanga Pepeta itafanya Show ya pili siku ijumaa Tarehe 2 Desemba 2011 katika mji wa Milton Keynes kwenye ukumbi wa Golden Lounge, Unit 35 Barton Road, Bletchley Milton Keynes.

Sunday, November 27, 2011

TANZIA

 FAMILIA YA MWAKIPUNDA WA NGAMANGA IPINDA KYELA MKOANI MBEYA WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MPENDWA WAO ANNEL MWAKIPUNDA MWAISUMO KILICHOTOKEA TAREHE 26/11/2011 DAR ES SALAAM. MAZIKO YATAFANYIKA MOROGORO TAREHE 28/11/2011
HABARI ZIWAFIKIE FAMILIA YA MWAKIPUNDA,FAMILIA YA MWAISUMO,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE NA MILELE
AMEN

WANAMITINDO WA KINYUMBANI WATINGISHA JIJI LA MARYLAND US



ILIVYOKUWA JANA KWENYE SHOO YA VINEGA a.k.a ANTVIRUS.

USIKOSE SHOO KALI KAMA HII.

Wednesday, November 23, 2011

AJALI MBAYA YA MAROLI YAUWA WATU BABATI.


Mafuta ya kupikia ya alizeti yalitapakaa katika eneo hilo.
 Walioteketea kwa moto inadhaniwa kuwa ni dereva na tandiboy waFuso ambao walibanwa katika gari hilo baada ya kukatika cabin.
Fuso ilivyoteketea kabisa na moto.
Watu zaidi ya wawili wanahofiwa kufa katika ajali ya gari iliyotokea usiku majira ya saa 6 katika eneo la kijiji cha Mdori Wilayani Babati Mkoani Manyara ambapo watu wawili walionekana miili yao ikiwa imeungua na moto. Ajali hiyo ililihusisha roli la mizigo lililokuwa limetokea Arusha na Fuso lililokuwa limetokea Singida.

Tuesday, November 22, 2011

LEO NI SIKU KUU YA KUZALIWA KWA HAWA RAFIKI ZANGU (ABDALLAH MWAIPAYA, GRACE MATATA NA MALIKIA RUTHA (Classic).

Abadallah Mwaipaya - Mtangazaji wa ITV / Redio ONE
Grace Matata - Msanii wa bongo Fleva
Malkia Ruta (Classic)
SULE'S INC. & ENTERTAINMENE pamoja na Blog ya MTOTO WA KITAA  na wasomaji wote wa blog hii wote kwa pamoja  tunampongeza marafiki hawa kwa sikukuu yao ya kuzaliwa leo.
Pia tunawatakia maisha marefu na yenye mafanikio kwa ujumla