b..

B1

Wynem

animation

Monday, January 31, 2011

GETHOKING AACHIA WANAPAGAWA

Msanii wa hip hop anaeweza kubadilika kutokana na mazingira hapa namzungumnzia mtu mzima GETHOKING sasa ameachia ngoma yake mpya ailiyoipa jiana la WANAPAGAWA ambayo ipo katika mahadhi ya ragamaphy huku akiwa amewashirikisha wasanii wawili wakali kabisa katika miondoko ya hip hop.
Akizungumza na mtoto wa kitaa GETHOKING alisema kwa sasa ameamua kuachia ngoma hiyo kwa kuwa watu wengi wamezoea kusema kuwa wana hip hop hawawezi kubadilika ndio maana ameiachia ili kuwaziba midomo "kaka mimi humu ndani nimedondosha maraga ya ukweli kabisa, na hii nimeifanya makusudi kabisa kwa sababu wabongo wengi wanasema kuwa wanahip hop hatuwezi kubadilika"
"mimi ningeweza kuchana lakini nimeamua kubadilika na nafasi ya kuchana nikawapa wanangu TEMBA na JOSE MTAMBO." aliongeza GETHOKING
GETHOKING pia aliwahi kukimbiza na songi zake kadhaa kama vile Kufa kiume, Msaliti aliewashirikisha Geez mabov na Rado, na My Birthday ambayo ipo kwenye video.

TUSHIRIKIANE KUIPELEKA MBELE HIP HOP NA SANAA YETU KWA UJUMLA.

GAZETI LAKO LA DIRA SASA LEO LIPO MTAANI KAMA KAWAIDA YAKE.

Kama kawaida GAZETI LAKO LA DIRAA YA MTANZANIA linalotolewa na kampuni ya DIRA MEDIA GROUP sasa limesheheni habari za uhakika zilizofanyiwa uchunguzi wa kutosha lipo mitaani leo kwa shilingi 500/- tu. Pata nakala yako sasa

Sunday, January 30, 2011

TIPELEKE WIKIENDI KWA NGOMA HII:- GOOD LOOK YA AY ft MISS TRINITY

BALOZI ARUDI KWENYE GEM KWA KISHINDO.


Ni miaka ya 90.Kitu tunachokiita hivi leo Bongo Fleva ndio kwanza kinaanza kushika kasi. Hakikubaliki bado. Wazazi wengi wanasema ni uhuni.Rap,Rap.Maanake nini? Vijana hawaeleweki mbele ya wazazi,ndugu,jamaa na hata baadhi ya marafiki. Yule keshapotea. Siku hizi kila ukikutana naye anarap-rap tu. Pamoja na hayo, zipo sehemu wanazokubalika. Kuna party za ufukweni. Huko wapo watu wanaowaelewa na kuwasikiliza achilia mbali kuwaona “idols”. Hawakukata tamaa. Wakaendelea kujitoa muhanga kwa kuelimisha kupitia sanaa ya muziki. Leo hii, muziki upo ulipo. Unasikilizwa na watu wa rika zote. Kampeni zinaendeshwa zikisindikizwa na muziki huo.
Miongoni mwa vijana waliokuwepo katika kundi hilo la ‘waasisi” ni pamoja na Ahmed Dola (pichani) ambaye kwa jina la kisanii, anajulikana kama Balozi Dola Soul. Bila shaka unamkumbuka toka enzi zile za The Deplomatz. Alitamba sana na nyimbo kama vile Kwenye ChatiNje ya Ndoa (akishirikiana na Mabaga Fresh) na zinginezo kibao.
Baada ya mafanikio kadhaa katika muziki ikiwemo tuzo ya kundi bora la Hip Hop akiwa na The Deplomatz mwaka 1999, Balozi aliamua kuhamishia makazi yake nje ya nchi akipitia nchi kama Uingereza na hatimaye Marekani alipo hivi sasa.
Je,amekacha game moja kwa moja? Jibu la wazi ni Hapana. He was busy taking care of other things such as school and family. Now he is back. Anawakumbusha wapenzi wa Bongo Fleva, toka katika generation yake mpaka hii mpya, kwamba bado anaweza na yupo tayari kurejea. Wimbo unaitwa Balozi Wenu.!!

Saturday, January 29, 2011

HIVI NI VITUKO USWAHILINI!



Mitaa ya Tandale Uzuri mchana huu mdada wa watu (ailiekaa chini) alijikua alkichezea kipndo kitakatifu baada ya kunywa bia za watu na kugoma kusepa na mchizi, baada ya baada ya kutembeza kipondo mchizi akaomna kukaa hapo ni kwere akaamua kijikataa (kuondoka) kiaina na inasemekana demu alikunywa bia za mvhizi huyo alieingia mitini na kukataa kuondoka nae. na jamaa alijikataa baada ya kuona nyomi limeshajongea pande hizo

Wasamalia wakijaribu kumstiri kwa mavazi baada ya yale ya kwake kuchafuka vibaya na kuchanika pia baada ya kipondo.

Msaada ukiendelea.

kina mama waliokuwepo eneo la tukio wakijaribu kumuinua mwanadada huyo aliekuwa ametembezea kipondo kitakatifu mchana huu.

Thursday, January 27, 2011

20% ALAMBA ZAWADI KUTOKA KWA MAN WATER.


John VN Shariza aka Man Water ambaye ndiye mmiliki wa Studio ya Combinations Sounds ambaye pia ndio Producer wa msanii wa 20 Percent.
Kufuatia kazi nzuri aifanyayo msanii wake Man Water mapema jana mchana aliamua kumsaprise msanii huyo kwa kumpeleka kwenye duka moja la vyombo vya mziki lililopo maeneo ya Kariakoo na kumnunulia vifaa kadhaa likiwemo gitaa.

"Nimemkabidhi zawadi hii ikiwa ni hatua ya kwanza na haikuwahi kutokea kwa Producer wa hapa bongo, kuonyesha kukubali kazi ya wasanii wao mpaka kutoa zawadi. Mimi nimeweka historia kwakua wa kwanza kufanya hivi na pia kuzidi kumpa support ya kusongambele katika muziki wake wa ndani na nje ya nchi.

Wednesday, January 26, 2011

VODACOM FOUNDATION KUMPIGA TAFU ALLY REHEMTULLAH KWENYE SAY NO TO DRUGS.



Ally rehemtullah kwa kushiriokiana na Vodacom Foundation wameungana katika shoo moja kaba,mbe ya kupinga utumiaji wa madawa ya kulevya mjini Zanzibar.
Show hii inatarajiwa kufanyika chini ya tamasha la kimataifa la sauti za busara ambapo shoo itafanyika tarehe 8 februarikatika hoteli ya Serena
Pia katika shoo hii itahusisha maonyesho ya mavazi kutoka kwa wanamitindo tofauti tofauti ambao ni Ally Reahemtullah, Vida Mashimbo, Farouk Abdala na kihanga huku wakiwa na mamodo kumi wtano wa kiume na watano wa kike wate wakiwa wametokea jiji Dar es Salaam.
 madansa wa kimatasifa wanaojulikana kama Tamaly Dalal watakuwepo katika kuipendezesha shoo hiyo
Ally Rehemtulla alisema wameamua kufanya onesho hilo kutopkana na uamuzi wao wa kusaidia upambanaji wa madawa ya kulevya na pia mapato yaote yatakayopatikana kwenye shoo hiyo yataenda katika shirika lisilo la kiserikali la Drug Free Zanzibar kwa ajili ya kusaidia mapambano ya madawa ya kulevya “mapato hii sho yetu yote yataenda katika kikundi cha Drug Free Zanzibar ambayo ni Ngo inayopambana na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Darling Hair, I-vew photogrpher, Valey spring na serena Hotel pia waejitokeza kuidhamini shoo hiyo.

HAYA NDIO MAMBO YA KITAA a.k.a KITAA KINAONGEA.

 
Mmenionaaaaaaaaaaaaaaaa!?!
Hapo vipiiiiiiiiiiii (picha zimefichwa sura kwa sababu maalum)

CHEKI VIDEO YA SHETTA FT BELLE 9 - NIMECHOKWA

Tuesday, January 25, 2011

TEKLA AACHIA NGOMA YA VALENTINE


Katika kukaribisha sikukuu ya wapendanao yaani valentain msanii wa kike kutoka M Lab TEKLA a.k.a TEK ameachia ngoma yake kali kabisa alioipa jina la NAFURAHI ikiwa imetangenezwa na pale studio za M Lab chini ya watayarishaji makini Nendeze & Kanye huku wakiongozwa kabisa na mtu mzima Duketachez wakati aditional vokal akiwa amesimama kijana Ben pol
Tekla ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa Tumaini univasity mwaka wa pili akichukulia kozi ya A mass communication a.k.a uandishi wa habari pia Tekla alipata kushirikiana na wasanii wengi kwa kuwaimbia koras a.k.a viitikio, nyimbo alizoshirikishwa Tekla ni kama ESHI LA MTU MMOJA by Fid Q, NYETI, USISHABIKIE VITU USIVYOVIJUA & RUSHWA by WAGOSI WA KAYA, BINTI KISURA by INSPECTOR Haroun na hizo ni chache tu!
na hii ngoma ya NAFURAHI ni ya pili kwa TEKLA tangu awe chini ya M LAB studio.
pia TEKLA anaomba sapot kwa mashabiki kwani wiki ijayo ataachia ngoma nyingine kali hivyo.

Gonga hapo pembeni kusikiliza ngoma mpya ya Tekla.

BASATA: WASANII PIMENI UKIMWI MTAMBUE AFYA ZENU.



Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari, BASATA, Godfrey Lebejo Mngereza akieleza juu ya haja ya wasanii kupima afya zao.
 Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Parapanda Mgunga Mwamnyenyelwa akionesha moja ya kazi zinazotazamiwa kufanywa na kundi lake hivi karibuni.
  
Mratibu wa Tamasha maarufu la Sauti za Busara linalotazamiwa kuanza Februari 9 mwaka huu Kwame Mchauru akichangia maoni kwenye Jukwaa la Sanaa.
Muelimishaji rika kutoka Shirika la AMREF, Bw. Bahati Mitula akitoa elimu kwa wasanii dhidi ya UKIMWI kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa BASATA. Baada ya elimu jumla ya wadau 107 wa Jukwaa la Sanaa walipata fursa ya kupima kwa hiari afya zao.



Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii na wadau wa sanaa kwa ujumla kujenga utaratibu wa kupima UKIMWI  mara kwa mara ili kutambua afya zao na baadaye kuweza kupanga mipango yao ya maisha na shughuli zao za sanaa.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari, BASATA George Lebejo Mngereza wakati wa zoezi maalum la kupima UKIMWI kwa hiari lililoendeshwa na program ya Jukwaa la Sanaa kwa kushirikiana na Shirika la AMREF kupitia mradi wa Angaza.
“Wasanii wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu wengine kupima UKIMWI huku wao wenyewe wakibaki nyuma wakati wako katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa,nadhani sasa wanapaswa nao kuwa mstari wa mbele katika kutambua afya zao ili sasa waweze kupanga mikakati katika shughuli zao za sanaa na maisha yao kwa ujumla” alisema Mngereza.
Aliongeza kwamba BASATA imekuwa ikitoa fursa mbalimbali za mafunzo dhidi ya UKIMWI kwa wasanii ambayo yamekuwa yakiambatana na zoezi la upimaji kwa hiari na lengo kuu la zoezi hilo ni kuwapa fursa wasanii ambao wamekuwa wakitumiwa kama daraja la kuhamasisha watu mbalimbali nao kufahamu kwa kina gonjwa hili na kujua jinsi ya kuliepuka lakini pia kutambua afya zao ili kuishi kwa tahadhari.
“Sote tutakumbuka kwamba Oktoba 25 mwaka jana BASATA iliendesha zoezi kama hili la elimu dhidi ya UKIMWI kwa wasanii na upimaji. Hii ni fursa nyingine kwa wasanii na wadau wa sanaa kwa ujumla kufanya hivyo ili kutambua afya zao” alisisitiza Mngereza.
Katika zoezi hilo ,jumla ya wadau 187 walihudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa ambapo kati yao  107 walipata fursa ya kupima kwa hiari na hakuna hata mmoja aliyekutwa ameathirika.Idadi hii ni ni zaidi ya wale wa zoezi lililopita kwani 79 tu ndiyo walipima.
Awali kabla ya zoezi la kupima, Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Parapanda Mgunga Mwamnyenyelwa aliwasilisha mada kuhusu Jinsi ya Kuifanya Sanaa na Utamaduni Wetu kutambulika kimataifa ambapo alisisitiza umuhimu wa wasanii wa muziki kuzingatia fani na maudhui ili kuweza kuzifanya kazi zao kuvuka kimataifa.
Aidha,alitumia fursa hiyo kutangaza tamasha kubwa la tamthiliya linalotazamiwa kuanza Januari 28 na kumaliza Januari 29, 2011 kwenye Ukumbi wa Utamaduni wa Ubalozi wa Urusi ambapo litahusisha wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari na baadaye wadau wengine.

Monday, January 24, 2011

KILI MUSIC AWARDS YAZINDULIWA RASMI.



Kutoka kushoto ni Mratibu wa Tunzo za Kilimanjaro kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Angelo Luhala, katikati ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe na Msaidizi wa KTMA Edith Bebwa wakiwa katika mkutano uliofanyika na waandishi wa habari hawapo pichani.
*********************************************
Na mwandishi wetu
Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro (Kilimanjaro Premium Lager) imezindua rasmi tunzi zake ambazo hutolewa kila mwaka wamesema mwaka huu watawatumia wasanii wa nyumbani katika kutoa burudani siku ya kilele cha hafla hiyo tofauti na ilivyokuwa katika miaka iliyopita ambako washereheshaji walikuwa ni wasanii kutoka nje.
Katika kunongesha zaidi onyesho hilo kubwa zaidi la utoaji tunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati , wasanii waliofanya vizuri mwaka jana tayari wametoa wimbo wao ambao waliutambulisha kwa wadau mwishoni mwa juma na utaanza kusikika katika vyombo mbalimbali ikiwa nikatika kuzitambulisha tunzo hizo kwa wadau kwamba kuna kitu kinakuja.
Tunzo hizo ambazo zinaratibiwa na Baraza la Sanaa Tanzania huku mdhamini wake mkuu tangu zianzishe ni TBL leo asubuhi wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kutoa tunzo kwa wasanii waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka jana.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya TBL ,Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema tunzo hizo zitatolewa kwa wasanii wa Tanzania ambao wamefanya vizuri kwa kupitia kazi zao za muziki walizofanya katika kipindi cha mwaka 2010.
Alisema tunzo hizo zimepangwa kutolewa katika hafla maalum itakayofanyika Machi 26 kawenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini.
Aidha Kavishe aliongeza kwa kusema wataendelea kufanya kazi na makampuni matatu katika mchakato wa utoaji tunzo na uwezeshaji wa tunzo za muziki huku akiyataja majina ya kampuni hizo kuwa ni Digital Arts ambao ni wasimamizi wa mawasiliano ya wasanii pamojana na umma.
Kampuni zingine ni One Plus Communications ambao nao ni wasimamizi ya wasanii pamoja na umma,Entertainment Masters watakaosimamia burudani na mahitaji yake kwa ujumla.
Kampuni nyingine ni Deloite Management Consulting ambao ni wasimamizi na wahakiki wa mchakato wa upatikanaji wa wateule pamoja na washindi wa tunzo nchini.
Ratiba ya mchakato huo inaonyesha Januari 19 walifanya uzinduzi kwa wadau katika hoteli ya nyota tano Double Tree Masaki, jana wamezindua kwa nahabari.
Februari 12 hadi 13 wataandaa jopo la wana Academy 100 katika hoteli ya Kunduchi Beach, Februari 16 watatangaza majina ya wasanii waliopitishwa kuwania tunzo.
Februari 21 wasanii waliochaguliwa watahudhuria semina ya siku moja na ifikapo Machi mosi ndipo kura zitaanzakupigwa kadhalika Machi 24 majaji watakutana na kuhakiki kura.
Kavishe aliongeza kwa kusema kuwa kura za wapenzi wa muziki nazo zitajumuishwa katika kuchagua washindi , mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitahesabiwa kwa asilimia 50 na majaji asilimia 50.Njia za kupiga kura ni kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno katika simu(SMS), Barua Pepe, Magazeti na Vipeperushi

GET YO COPY OF DIRA NEWS PAPER TODAY.

Gzeti la DIRA ya mtanzania ambalo hutolewa na kampuni ya Dira Media Group na kusambazwa kila juma tatu sasa limeboreshwa kwa limeongezwa kurasa kutoka kurasa 16 mpaka kurasa 24. kama kawaida

MSHINDI MISS UTALII TANZANIA 2010- 2011 KUNYANYUKA NA SH. MILIONI MIA MOJA HAMSINI



Baadhi ya washiriki Miss Utalii Tz- 2010- 2011wakila tizi katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar, Jumapili
Washiriki Miss Utalii Tz- Kusini na Magharini kabla ya mchezo

Mbunge wa Kinondoni Idd Azan akisalimiana na washiriki wa Miss Utalii Tz Kaskazini wakati wa Mchezo wa Kirafiki Dhidi ya warembo wa Mashariki
Baadhi ya washiriki wa Miss Utalii Tz- 2010- 2011 katika mazoezi kabla ya Michezo ya wao kwa wao katika ufukwe wa Coco Beach
Juu na chini washiriki wa Miss Utalii Kanda ya Mashariki na Kaskazini wakichuana katika michezo ya Soka ya Ufukweni Coco Beach jana.
Wakati fainali za taifa za shindano la Miss Utalii Tanzania zimepangwa kufanyika usiku wa Februari 5, 2011, mrembo atakayenyakua taji la taifa la Miss Utalii mwaka huu ataondoka na faida kubwa ya zawadi ya mkataba wenye thamani ya shilingi milioni mia moja na hamsini.
Na Mwandishi wetu
Taarifa iliyotolewa na Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo imeeleza kuwa, shindano la mwaka huu litafanyika kwenye hoteli ya kitalii ya Kiromo View Resort iliyopo umbali wa kilometa kumi tu toka Bagamoyo mjini ambapo pia kutakuwa na burudani kadhaa zitakazosindikiza usiku huo adhimu na ya kihistoria katika tasnia nzima ya urembo na utalii hapa Tanzania.
Akaendelea kusema; washiriki wote wa fainali za Miss Utalii Tanzania 2010/11 wako katika hali nzuri kiafya na kisaikolojia kwa ajili ya shindano na kufafanua kuwa mbali ya kitita hicho kwa Malkia wa mwaka huu, warembo wengine wataweza kujitwalia mataji yatakayowakilisha hifadhi za taifa 16 zilizo chini ya mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kadhalika, Chipungahelo amesema kuwa mbali ya mataji ya hifadhi, pia, kutakuwa na tuzo zingine toka baadhi ya makampuni na taasisi zilizodhamini shindano hili ili kuyawakilisha katika suala zima la kuutangaza utalii kupitia hifadhi za taifa na utamaduni wa Mtanzania na hivyo kuongeza hamasa zaidi kwa washiriki ambao nao wameonesha kujawa shauku ya kufanya vema.
“Fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2010/11, zitakuwa tukio kubwa zaidi la kitaifa la kitamaduni na urembo nchini, ambalo kishindo chake kitaleta mageuzi makubwa katika sanaa ya urembo nchini, barani Afrika na duniani kwa ujumla. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa mara ya kwanza dunia itashuhudia idadi kubwa ya warembo wakiwa jukwaa moja wakitangaza na kuonesha utamaduni kupitia mavazi ya asili, ya kitalii, ya mitindo, ya ubunifu. Pia, warembo hao wataonesha vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za mikoa au kanda wanazowakilisha,’ amesema Rais wa Miss Utalii Tanzania.
Aidha, amewataja wadhamini wakuu wa shindano la taifa la Miss Utalii 2010/11 ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Business Times Limited, Kiromo View Resort na Sahara Media Group Limited,inayomiliki kituo cha runinga cha Star TV, Radio Free Africa, Kiss FM na gazeti la Msanii Afrika.Wengine ni Zizzou Fashion, Alaisy Travel, Auckland Tours, Tintona TankStation, Tesco Furniture, Mlonge By Makai Enterprises,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Coco Beach.
Warembo hao wameanza ziara rasmi za kutembelea na kutangaza vivutio vya utalii ,kwa kutembelea maeneo ya kihistoria yaliyopo Mkoani Pwani,ambapo juzi walitembelea Maeneo ya Kihistoria yaliyopo wilayani Bagamoyo ikiwemo Magofu ya Kaole,wakiongozwa na katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo.
Aidha jana warembo wote 60 walitembelea na kutangaza Fukwe za Bahari ya Hindi zilizoko mkoani Dar Es Salaam wakiongozwa na Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan. wakiwa katika Fukwe wa Coco Beach warembo hao wakiwa wamegawanywa katika timu nne za mpira wa miguu walishindana kusakata kabumbu la Ufukweni hali iliyopelekea kuwa kivutio kikubwa na kusababisha ufukwe huo kufurika mamia ya watu wakishuhudia warembo hao wakionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kandanda.
Michuano baina ya timu hizo za warembo zilizopewa majina ya hifadhi za Taifa ulikuwa mkubwa na kuamsha shangwe za mara kwa mara kwa wapenzi waliojazana kushuhudia mechi hizo. katika mchezo wa kwanza timu ya soka ya warembo wa Ngorongoro iliweza kuibwaga timu ya soka ya Selous kwa mabao 4-2 wakati katika mchezo wa pili ambao ulizikutanisha timu za Serengeti National Park dhidi ya Maunt Kilimanjaro na matokeo timu ya Mlima Kilimanjaro kuibuka kwa ushindi wa mabao 3-1.
Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan kwa kufurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na timu hizo za warembo wa miss Utalii Tanzania 2010- 2011 ambao tarehe 5 mwezi wa pili watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2010- 2011 katika Hotel ya Kitalii ya Kiromo Bagamoyo, alinunua kila goli kwa shilingi elfu kumi(10,000) hivyo aliweza kutoa shilingi laki moja kwa magoli kumi yaliyofungwa. naye mfanyabiashara maarufu nchini Zizzou Fashion alitoa seti nne za jezi kwa warembo wote 60

SAUTI ZA BUSARA AROUND DA CONER.


Djaaka was founded in Beira, Mozambique in 2001 by members from the big traditional music and dance company “Companhia de música e dança traditional da Beira”. Not long after their formation they won the regional young musicians’ festival Music Crossroads in 2002. It was here that they gained substantial regional exposure, winning several prizes, one of which was a visit to Fallun, the folk music festival in Sweden.

Their music reflects various traditions from central Mozambique. Djaaka’s sound can be identified largely by their use of marimba which comes from one area of central Mozambique called “Timbila” is heard on many of their songs. The music is contemporary with a strong traditional touch, both funky and deeply rooted. Djaaka sing in a dialect called Massena, which is not far removed from languages of Zambia, like Bemba and Njanja.

Djaaka is a true live band, skilled musician and good dancers, with outstanding outfits. Their live performance has impressed not only their home audience; it has brought them to festivals in Reunion, Mauritius, South Africa, Zimbabwe, Italy and United Kingdom. They have won the “best Mozambican band” award three times at TOP-Ngoma, held by Radio Mozambique.

Friday, January 21, 2011

KAKA ZAO KURUDI UPYA KWENYE GEMU


Kaka zao ni family inayotengenezwa na watu watano kutoka kanda ya ziwa mwanza. ambao ni Hardmad  mkushi a.k.a KIDUME akiwa kama kiongozi na Phantom ranks ambaye kwa sasa yuko nchini uswisi, wengine ni Fatma kilometa, Jahson pamoja na Susu.Tunafanya mziki aina ya dancehall na raga rumba.
Kwasasa makazi yetu ni hapa Dar es salaam kwa ajiri ya shughuli zetu za muziki.
Jahson ameachia Track pamoja na video inayoitwaHEAT akiwa na Hardmad na kwa sasa huko anafanya nyimbo nyingine inayoitwa SHOW ME SOME LOVEakiwa na Susu pamoja na Fatma. Hivi karibuni itakuwa hewani.
Big up sana kwa mashabiki wanaotupa suport pia big up kwa wapenzi wa dancehall pamoja sanaaaaaaaaaaaana
 R whu jah bless no man cian tes

Tuesday, January 18, 2011

CBH AACHIA NGOMA TATU KWA MPIGO.

Baada ku kutamba na vngoma ya ke ya Best Friend kwenye Oudio na Video msanii CBH watu walidhani amebahatika lakini kwa sasa anaonesha uwezo wake baada ya kuachia ngoma tatu kali zote zikiwa kwenye stail ileile kama aliyotoka nayo mwanzo. ngoma alizotoka nazo CBH ni
am in love, Broda na oweeeoh.
CBH kwa sasa anasimamiwa na kampuni ya muziki ya SHOW BIZ DIFINE chini ya mtu mzima Eyryn D.

Monday, January 17, 2011

BASATA LEO PALIKUWA HAPATOSHI

Katibu mtendaji wa baraza sanaa la taifa (BASATA) Ghonche Materego 
Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akiongea jambo kwenye jukwaa la sanaa
Hili ndio nyomi lililokuwepo pale kwenye jukwaa la sanaa kwenye ukumbi wa basata

Hawa ni baadhi ya wadau wakichangia mada iliyokwa ikizungumziwa.
Mrisho Mpoto akihojiwa na mwandishi wa habari mara baada ya kikao kuisha
Na hapa ni zamu ya Mkoloni kuhojiwa na mwandishi mara baada ya kikao kuisha

Sunday, January 16, 2011

MSIKILIZE NA MUONE MH. JOHN MNYIKA KATIKA KONGAMANO LA MCHAKATO WA KATIBA MPYA.

GAZETI LAKO LA DIRA LIPO MITAANI TENA LEO.


Kama kawaida gazeti lako la DIRA lipo miataani leo hii likiwa limesheheni habari zilizofanyiwa uchunguzi na kuhakikiwa kwa umakini kabia. linapatikana kwa Tsh. 500/= tu. Pata kopi yako mapema usikubali kuukosa uhondo huu.

BENJAMINI WA MAMBOJAMBO BADO YUKO CHIMBO.

Leo nimepokea meseji kutoka kwa kaka bjamini wa mammbojambo akisema kwamba wadau wasimuone kama kakaa kimya sana ila ni kwa sababu yuko chimbo anaandaa albamu.mesji ilkua hivi......
"mambo vipi kaka a.k.a Mtoto wa kitaa! naomba unisaaidie kuwaambia mafans wangu kuwa wasijali na wala wasiogope kwa mimi kukaa kimya, sasa hivi nipo chimbo naandaa ngoma kalikali ambazo zitawarusha kiuhakika,pia ndio naandaa albam yangu ambayo nategemea kuiachia kitaani mwezi mei, na cha mwisho napenda kuwaambia mashabiki na wapenzi wa muziki wangu kuwa bado nipo nao kwa kila kitu kwani Benjamini ni yuleyule wa siku zote ambae anawapa vitu vikali siku zote."
Mesiji iliishia hapo. Sule's Inc. & entertainment  inamtakia Benjamini Mafanikio mema katika harakati za kuupeleka huu muziki wetu mbele. 2PO PA1

Thursday, January 13, 2011

USIKU WA BEN POUL WITH THE M BAND LEO


WELCOME TO THE MUSIC NIGHT WITH THE M BAND EVERY THURSDAY @BUDHABLU LOUNGE MIKOCHENI NEAR DR. KAIRUKI'S HOSPITAL, FROM 8:00pm TILL 00:00pm, THIS THURSDAY BEN POL WILL BE PERFORMING LIVE WITH THE M BAND, Tsh. 5000 @ THE GATE.

BASATA YAUKARIBISHA MWAKA KWA KISHINDO KATIKA SEKTA YA SANAA

Afisa wa Sanaa za Maonyesho kutoka BASATA Rajab Zubwa (Kulia) akilicharaza gitaa huku Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi (Kushoto) na Katibu wake wakisakata
Baadhi ya wafanyakazi wa BASATA wakiinamisha vichwa kwa dakika moja kwenye hafla ya kuukaribisha mwaka 2011 kama ishara ya kuwakumbuka wasanii na wadau wa sanaa waliotutoka katika kipindi cha mwaka wa 2010.
Wafanyakazi wa BASATA pamoja na baadhi ya wageni waarikwa wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kupata maakuli.
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa BASATA wakiyarudi magoma.Hakika ilikuwa ni furaha.

Na Mwandishi Wetu

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wiki hii limefanya hafla fupi ya kuukaribisha mwaka huku Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Ghonche Materego akiwatangazia wafanyakazi kwamba,mwaka huu wa 2011 ni wa kazi na kasi kubwa katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya sanaa.
Materego alianika mikakati iliyopo kuwa ni pamoja na kuhakikisha ukumbi mkubwa wa burudani wenye uwezo wa kuchukua watu 1,000 unakamilika, tamasha kubwa la siku ya msanii wa Tanzania linafanyika kwa mafanikio makubwa, mashirikisho ya sanaa nchini yanafanya kazi kwa ufanisi na kiwango cha juu na mikakati mingine mingi.
“Mwaka huu lazima tufanye kazi kwa kasi na kiwango kikubwa,lazima ukumbi wetu wa BASATA umalizike kwa hali na mali,tamasha kubwa la msanii wa Tanzania lifanyike kwa mafanikio.Ni mwaka wa kuleta mabadiliko kwenye sekta yetu ya sanaa” alisisitiza Materego.
Aliwaasa viongozi wa mashirikisho ya sanaa nchini waliohudhuria hafla hiyo kwa niaba ya wasanii wote nchini kwamba, lazima wahakikishe wanawaunganisha wasanii katika kupigania maslahi na hki zao na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea lakini kubwa kuhakikisha mchango na takwimu sahihi za sekta ya sanaa zinapatikana.
Akiongeza zaidi alisema “Changamoto tuliyonayo mbele ni ya kuwa na takwimu sahihi katika sekta yetu ya sanaa.Kwa muda mrefu sekta yetu imekuwa ikifichwa kwenye sekta nyingine hivyo mchango wake kwenye pato la taifa kutokutambuliwa moja kwa moja.Ni wajibu wetu sasa kuhakikisha tunakuwa na takwimu sahihi za sekta hii.
Hafla hiyo fupi ya BASATA ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2011 ilifanyika kwenye viwanja vya baraza hilo na kuhudhuriwa na wafanyakazi wote,viongozi wa mashirikisho ya sanaa nchini na uongozi wa juu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Burudani.